Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania yapiga hatua ugunduzi mafuta

Muktasari:

  • Uchukuaji na utafsiri wa takwimu za kijiokemia zilizoonyesha uwepo wa viashiria vya miamba vyenye uwezo wa kuzalisha mafuta au gesi kwenye kitalu cha Eyasi wembere kilichopo bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki umekamilika.

Dar es Salaam. Tanzania imekamilisha uchukuaji tafsiri za takwimu za kijiokemia zilizoonyesha uwapo wa viashiria vya miamba vyenye uwezo wa kuzalisha mafuta au gesi katika kitalu cha Eyasi Wembere.

Kwa upande wa gesi, Tanzania inakadiriwa kuwa na mita za ujazo wa gesi asilia trilioni 230 japo ni futi trilioni 57.5 zimethibitishwa mpaka sasa.

Tayari gesi hiyo imeanza kuchimbwa kwenye visima vya Songosongo wilayani Kilwa na Msimbati mkoani Mtwara.

Utafiti bado unaendelea kufanyika kwenye eneo la mafuta ambapo mpaka sasa taarifa za awali zinaonyesha huenda Tanzania ikagundua nishati hiyo.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kining’inila kilichopo Wilaya ya Igunga hivi karibuni Mjiofizikia wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) Sindi Maduhu amesema kwa mwaka wa fedha 2023/24 Serikali imetoa Sh8 bilioni kukamilisha hatua za awali za utafutaji wa mafuta kwa njia ya mitetemo ya mfumo wa 2D,

Kufuatia shughuli hizo, Shirika limeendelea kutekeleza mkakati wa kuelimisha wananchi wanaoguswa na mradi huo kwenye mikoa yote mitano na wilaya sita za Karatu, Igunga, Meatu, Mkalama, Iramba na Kishapu   kwa lengo la kuwajengea uwezo wananchi kuelewa shuhghuli za mradi, ulinzi na usalama na kutambua fursa zinazoambatana na mradi huo.

Akiongea na wananchi katika kijiji cha Kining’inila kilichopo wilaya ya Igunga Mjiofizikia Sindi Maduhu aliwaeleza wananchi kuwa kwa mwaka wa fedha 2023/24, Serikali imetoa fedha kiasi cha shilingi bilioni nane (8) ili kukamilisha hatua za awali za utafutaji wa mafuta kwa njia ya mitetemo ya mfumo wa 2D,

Nawaomba wananchi msiwe na hofu, mtoe ushirikiano kwa wataalamu watakaokuwa wakipita maeneo yao ili zoezi hili likamilike kwa wakati.

Pia msiwe na hofu wataalamu wa utafutaji watakapofika kwenye maeneo yenu kwani tafiti hizi huambatana na kuwepo kwa kifaa cha kurekodia mitetemo vinavyoitwa ‘Node’ na magari makubwa ambayo hutumika kuzalisha mitetemo na hataye kupata taarifa za miamba,”amesema.

Maduhu amesema TPDC itaendelea kutekeleza mkakati wa kuelimisha wananchi wanaoguswa na mradi huo kwenye mikoa yote mitano na wilaya sita za Karatu, Igunga, Meatu, Mkalama, Iramba na Kishapu   kwa lengo la kuwajengea uwezo wananchi kuelewa shuhghuli za mradi, ulinzi na usalama na kutambua fursa zinazoambatana na mradi huo.

Hayo yanasisitizwa na Ofisa Maendeleo ya Jamii wa TPDC Oscar Mwakasege akiwa kijiji cha Isakamaliwa kilichopo kata ya Isakamaliwa –Igunga ambaye amewataka wananchi kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama wa mali za wakandarasi wakati wa shughuli za utafutaji wa mafuta.

“Katika kuongeza wigo wa utoaji elimu shule mbalimbali zilifikiwa kupatiwa elimu,hatua ya kuwafikia wanafunzi ni muhimu sana kwani wanafunzi wakiwa na uelewa  watafikisha ujumbe kwa ndugu, jamaa  na jamii kwa ujumla   kwa idadi kubwa,”amesema.

Kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo, Mwenyekiti wa kijiji cha Kinging’inila  Christopher Zengwe ametoa rai kwa wananachi kushirkiana kuulinda mradi ikiwa ni pamoja na kutoa ushirikiano kwa watafiti na kuchangamkia fursa zitakazoambatana na mradi huo kama ajira za muda mfupi na muda mrefu.

Naye Steve Wawa mnufaika wa ajira katika kambi ya muda ya utafutaji mafuta iliyopo kijiji cha Bukundi wilayani Meatu amesema mradi huo umemsaidia kupata fedha za kutimiza mahitaji ya familia yake pamoja na kuendesha maisha ya kila siku ikiwa ni pamoja kusomesha watoto wake.

Mradi wa utafutaji mafuta na gesi asilia kitalu cha Eyasi Wembere ni miongoni mwa miradi ya kielelezo ya Taifa iliyoainishwa kwenye Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka mitano 2021 hadi 2026) inayotekelezwa na Serikali kupitia TPDC.

Sughuli za utafutaji wa mafuta katika eneo hilo zilianza mnamo 2015, ambapo taarifa zenye urefu wa kilomita 11,323 za uzani na usumaku zilichukuliwa na taarifa za kijiolojia za miamba, uchorongaji wa visima vifupi vitatu kwa ajili ya kutambua miamba yenye viashiria vya uwepo wa mafuta/gesi asilia.