Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania yaomba ahueni ya uhaba wa dola kwa Benki ya Dunia

Muktasari:

  • Serikali ya Tanzania imekutana na Benki ya Dunia, huku upungufu wa Dola ya Marekani likiwa moja ya mambo yaliyojadiliwa katika majadiliano hayo.

Dar es Salaam. Ili kulinda ukuaji uchumi na kuepuka athari za kupanda kwa gharama za maisha, Tanzania imejadiliana na Benki ya Dunia juu ya namna itakavyosaidiwa kukabiliana na athari za upungufu wa Dola ya Marekani katika mzunguko wa fedha.

Majadiliano hayo yanakuja, katikati ya wimbi la kupungua kwa sarafu hiyo duniani kunakotajwa kuchagiza ongezeko la bei ya baadhi ya bidhaa muhimu yakiwemo mafuta.

Tayari uhaba wa sarafu hiyo, umeacha makovu katika bei ya mafuta kulingana na taarifa ya jana ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura).

Taarifa hiyo, imeeleza katika Jiji la Dar es Salaam bei ya Petroli imepanda kwa Sh14 huku dizeli ikipanda kwa Sh324.

Pamoja na majadiliano ya kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na benki hiyo, msaada wa kukabiliana na kupanda kwa sarafu hiyo ni jambo lingine lililojadiliwa.

Majadiliano hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam leo, Septemba 6, 2023 ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Dk Mwigumu Nchemba, huku Benki ya Dunia ikiwakilishwa na Mkurugenzi wake anayesimamia kanda ya mashariki na Kusini mwa Afrika, Hassan Zaman.

"Masuala mbalimbali yamejadiliwa ikiwemo namna ya kuisadia nchi kukabiliana na athari za upungufu wa Dola za Marekani katika mzunguko wa fedha, ili kulinda ukuaji wa uchumi," imeeleza taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu majadiliano hayo.

Katika majadiliano hayo ameiomba benki hiyo, kuharakisha upatikanaji wa zaidi ya Dola za Marekani 500 milioni ifikapo Novemba mwaka huu.

Ameeleza fedha hizo zitaisaidia nchi kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa sarafu hiyo katika mzunguko wa fedha nchini hali inayochangia mfumuko wa bei na kukwamisha uagizaji wa bidhaa muhimu kutoka nje ya nchi yakiwemo mafuta.

Hata hivyo, Dk Nchemba ameeleza mipango ya Serikali kuboresha mazingira ya biashara ili kuiwezesha sekta binafsi kuchangia ukuaji uchumi.

Hatua hiyo, amesema itachagiza kuwezesha upatikanaji wa fedha za kigeni kupitia uwekezaji wa mitaji kutoka ndani na nje ya nchi.

Kwa mujibu wa Dk Nchemba, mabadiliko mbalimbali ya sheria yameshafanyika na mengine yanaendelea ili kuvutia uwekezaji wa mitaji na teknolojia.

Alitumiwa fursa hiyo, kuishukuru Benki ya Dunia kwa kuidhinisha upatikanaji wa fedha kwenye miradi nane yenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani 2.16 bilioni.

Akizungumza katika majadiliano hayo, Zaman amepongeza hatua za Serikali za kukuza uchumi licha ya uwepo wa janga la Uviko-19.

"Nchi nyingi za Afrika zinapaswa kujifunza kutoka Tanzania kuhusu usimamizi wa sera za fedha na uchumi," amesema.