Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania yakwama hoja mbili ikipinga fidia ya Sh300 bilioni

New Content Item (1)

Muktasari:

  • Serikali iliwasilisha hoja hizo baada ya ICSID  Julai 2023 kutolewa hukumu hiyo, hivyo walitaka Mahakama kuifuta inayoelekeza kulipa fidia ya Dola 109 milioni za Marekani (Sh272 bilioni) ya Kampuni ya Indiana Resources (IDA).

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imekataliwa hoja  mbili kati ya tatu ilizowasilisha  Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) kukwama.

Serikali iliwasilisha hoja hizo baada ya ICSID  Julai 2023 kutolewa hukumu hiyo, hivyo walitaka Mahakama kuifuta inayoelekeza kulipa fidia ya Dola 109 milioni za Marekani (Sh272 bilioni) ya Kampuni ya Indiana Resources (IDA).

Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa ya ICSID hela hiyo imefikia Dola 113.9 milioni za Marekani (Sh282 bilioni) pamoja na gharama za ziada za Dola 4.2 milioni (Sh10.5 bilioni) zikiwa na jumla ya Sh292 bilioni.

Kwa mujibu wa hukumu hiyo, riba ya Dola 1 milioni za Marekani (Sh2.5 bilioni) itaongezeka kila mwezi hadi Tanzania itakapolipa kiasi hicho au Indiana itakapozuia mali ya Tanzania itakayoendana na thamani ya madai hayo.

Desemba 2023, Mwanasheria Mkuu wa Tanzania alitoa barua ya uthibitisho kwa ICSID kwamba, nchi ingelipa bila masharti na bila kubatilishwa kiasi chote cha fedha hiyo ndani ya siku 45 baada ya uamuzi wa mwisho wa kubatilisha.

Hata hivyo ni takribani miezi miwili sasa tangu hilo litokee.

Baada ya ICSID kukataa mapendekezo mengi ya Tanzania ya kuomba kubatilishwa kwa hukumu hiyo tulimtafuta Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, Dk Eliezer Feleshi aeleze Serikali itafanya  nini baada ya hayo.

Dk Feleshi amesema, “hatuko tayari kuzungumzia jambo ambalo liko kwenye meza ya usuluhishi na uamuzi wake wa mwisho haujafikiwa.”

Msingi wa madai hayo unatokana na ukiukwaji wa Mkataba wa Uwekezaji (BIT) uliosainiwa kati ya Serikali na UK & Ireland ya Kaskazini mwaka 1994, unaohusisha wanahisa wenza wa Indiana Resources waliomiliki leseni hiyo.

Kwa mujibu wa Indiana, wanahisa waliishawishi Serikali kurejesha leseni yao, lakini haikuwezekana kutokana na marekebisho ya Sheria ya Madini ya mwaka 2017 yanayoelekeza kuzifuta.

Indiana inanufaika na fidia hiyo kutokana na umiliki wa asilimia 62.4 ya hisa za kampuni mbili (Ntaka Nickel Holdings Ltd na Nachingwea UK Limited) zilizokuwa zikimiliki leseni ya kuhodhi ardhi katika eneo la Mradi wa Nikel wa Ntaka Hill, uliokuwa Wilaya ya Nachingwea.

Mwenyekiti Mtendaji wa IDA, Bronwyn Barnes amesema uamuzi huo ni matokeo mazuri sana kwa walalamikaji.

“Tumekuwa tukisisitiza kwamba nyaraka zilizowasilishwa na Tanzania hazionyeshi kwamba itaweza kukidhi viwango vya kufuta hukumu hiyo, na uamuzi huu wa hivi karibuni kutoka ICSID unathibitisha hilo,” Barnes amesema.

Tanzania ipo kwenye mikataba ya uwekezaji baina ya nchi mbili (BIT) na nchi 18 duniani lakini 10 inayofanya kazi ni ya Italia, Denmark, China, Mauritius, Ujerumani, Uingereza, Finland, Sweden na Uturuki, Uholanzi na Uswisi (imevunjwa).

Kwa mujibu wa chambuzi za mtandao wa asasi za kiraia na vyama vya wafanyakazi unaofanya chambuzi za biashara sera na uwekezaji (Tatic), Tanzania imejikuta ikilipa zaidi ya Sh1.5 trilioni kutokana na kuvunja mikataba na baadhi ya kampuni wa nchi zilizo na mikataba nayo.

Kesi ya hivi karibuni ni ya Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Winshear Gold Corp,  Serikali ilidaiwa kuingia makubaliano kuilipa Dola 30 milioni za Marekani (Sh75 bilioni) ili kumaliza kesi hiyo.

Kesi nyingine ni ya Sunlodges (T) Ltd dhidi ya Serikali ya Tanzania.

Sunlodges BVI ilishinda kesi hiyo na kutakiwa kulipwa Dola 8.91 milioni za Marekani (Sh22.34 bilioni) ikiwa na asilimia ya riba kwa mwaka kuanzia Septemba 5, 2011 na ilitakiwa kulipwa ndani ya siku 60.

Serikali ya Tanzania ililipa Sh50.1 bilioni mwaka 2021 kumaliza kesi hiyo.