Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania mjumbe Skauti wa kike duniani

Kamishna wa Mafunzo Chama cha Skauti wa Kike Tanzania Dk Helga Mutasingwa, ambaye amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Bodi Jumuiya ya Skauti wa Kike Duniani (WAGGGS)

Muktasari:

  • Miongoni mwa faida watakazozipata vijana wa kike wanaohimizwa kujiunga na Skauti ni kupata mafunzo ya afya, mazingira, usawa wa kijinsia na kujiboresha kiuchumi.

Dar es Salaam. Kwa mara ya kwanza, sasa Tanzania ni mjumbe wa bodi, Jumuiya ya Skauti wa Kike Duniani (WAGGGS), hii inatokana na Kamishna wa Mafunzo wa Chama cha Skauti wa Kike Tanzania (TGGA), Dk Helga Mutasingwa, kuchaguliwa kuingia kwenye bodi hiyo, katika mkutano wa chama hicho nchini Cyprus.

Akizungumza mara baaya ya kuwasili nchini kwa mjumbe huyo wa bodi, Kamishina Mkuu wa TGGA, Marry Richard, amesema nchi imepata heshima kubwa.

“Ni Skauti wa kwanza kutoka Tanzania kuchaguliwa nafasi hiyo, hivyo hii ni mara ya kwanza Tanzania inapata uwakilishi kwenye chombo hicho kikuu cha maamuzi cha Chama cha Skauti wa Kike duniani, hii ni heshima kubwa kwa nchi,” amesema Kamishna Mkuu Marry na kuongeza;

“Hii ni fursa ya kiuongozi leo hii tumepata mjumbe kwenye bodi ya dunia ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa nchi yetu hivyo mtoto wakike ni kiongozi."

Kwa upande wake Dk Helga amehimiza vijana wa kike nchini kujiunga na chama hicho kwaajili ya kujipatia fursa mbalimbali ikiwemo uongozi, kwani mtoto wa kike anauwezo hivyo anapaswa aendelezwe.

“Tunampatia nafasi mtoto wa kike haijalishi ana umri gani, cha msingi tutashirikiana kwaajili ya kupata mafunzo ya mazingira, kuboresha uchumi, afya na uongozi,” amesema Mutasingwa.

Dk Mutasingwa, amesema skauti hao watajitolea katika jamii sambamba na kujiweka karibu na nafasi za kiuongozi jambo ambalo litawapatia heshima zaidi.

“Tunashirikiana katika kujifunza wote lengo likiwa ni kuisadia jamii inayotuzunguka kwa kushirikiana na Serikali, haijalishi awe shule awe anafanya kazi hatubagui,” ameweka wazi.