Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania kuuza umeme nje ya nchi kuanzia mwakani

“Mipango yetu ni kwamba ifikapo mwaka 2014 tayari tutakuwa na umeme wa ziada kiasi cha megawati 500 ambao tutauuza nje ya nchi.”

Muktasari:

  • Hayo yalibainishwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ambaye alikuwa akizungumza kabla ya kusainiwa kwa makubaliano ya maelewano baina ya Shirika la Umeme Tanzania  Tanesco na Kampuni ya kuzalisha umeme ya China Power Investment (CPI).

Ni kauli ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter  Muhongo  alipozungumza jana.

Dar es Salaam. Tanzania inakusudia kuanza kuuza umeme nchi za nje kufuatia mapinduzi yanayotazamiwa kufanyika kwenye sekta ya nishati na madini ukiwamo uendelezwaji wa mradi wa uzalishaji umeme katika eneo la Kinyerezi.

“ Mipango yetu ni kwamba ifikapo mwaka 2014 tayari tutakuwa na umeme wa ziada kiasi cha megawati 500 ambao tutauuza nje ya nchi, ilielezwa jana.

Ili kufikia azma hiyo, Wizara ya Nishati na Madini imebainisha maeneo ambayo inatazamia kuyawekea mkazo ili kuzalisha umeme wa kutosha. Maeneo hayo ni pamoja na uendelezwaji wa nishati ya gesi inayotazamiwa kuanza kuchimbwa mkoani Mtwara pamoja na utumiaji wa makaa ya mawe.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ambaye alikuwa akizungumza kabla ya kusainiwa kwa makubaliano ya maelewano baina ya Shirika la Umeme Tanzania  Tanesco na Kampuni ya kuzalisha umeme ya China Power Investment (CPI).

Waziri Muhongo alisema kuwa,  Serikali pia inakusudia kuimarisha vyanzo vingine vya uzalishaji umeme ambavyo vitajumuisha umeme utokanao na upepo, jua na maji.

Alisema kuwa, shabaha ya Serikali ni kuendelea kukuza uchumi wa taifa kwa kiwango cha kuanzia asilimia 8 na kwamba kiwango hicho kitakuwa kimekuwa hadi kufikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2015.

“ Ili kufanikisha lengo la kuendelea kukuza uchumi, inatupasa kuhakikisha kwamba tunakuwa na umeme wa uhakika….

 Hii mipango yetu itahakikisha tunaondokana na tatizo la umeme na kusema kweli tunakadiria kwamba ifikapo mwaka 2015 tutakuwa na kuwango cha kutosha cha umeme wa ziada, hatua ambayo itatufanya tuuze kiasi kikubwa umeme”

Alisema kuwa kutokana na mipango iliyoandaliwa na Serikali, kuanzia sasa umeme utachukuliwa kama bidhaa ambayo itatafutiwa masoko katika nchi za nje na kuuzwa.

Katika hatua nyingine, Shirika la Umeme nchini Tanesco limeingia katika makubaliano na kampuni ya kuzalisha umeme ya China Power Investment kwa ajili ya kuendeleza mradi wa uzalishaji wa umeme katika eneo la Kinyerezi.  Mradi huo ambao unaingia hatua ya tatu kati ya nne zilizopangwa utakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme kiasi cha megawati 600.

Kwa mujibu wa Waziri Muhongo, kukamilika kwa miradi hiyo ikiwamo usafirishaji wa gesi kutoka mkoani Mtwara  kutasaidia kufungua soko la ajira hatua ambayo itakuwa fursa njema kwa vijana.