Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanapa kufunga kamera za kudhibiti mwendo Mikumi

Ofisa Uhifadhi, Herman Mtei

Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) liko mbioni kufunga kamera za kuangalia vyombo vya moto ambavyo vinakwenda mwendo wa kasi na kusababisha vifo vya wanyama kwenye Hifadhi ya Mikumi barabara inakopita katikati.
Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi Machi 23, 2023 mkoani Morogoro na Ofisa Uhifadhi, Herman Mtei alipokuwa akiwaeleza wahariri mipango ya Tanapa kulinda wanyama katika hifadhi hiyo.
Amesema taratibu zilizopo kwenye hifadhi hiyo kila gari linaruhusiwa kuendeshwa kwa spidi 50 kwa saa lakini watumiaji wa barabara inayopita kwenye hifadhi huendesha vyombo vyao kwa zaidi ya kiwango hicho.
Amesema kila mwaka zaidi ya wanyama 700 wanakufa kwa kugongwa na magari yanayoendeshwa kwa spidi zaidi ya 50.
“Tutaanza kutumia zaidi teknolojia katika kudhibiti vifo vya wanyama vinavyotokana na ajali zinazosababishwa na mwendo wa kasi. Sasa utakapoingia kwenye mbuga yetu kutakuwa na geti ambalo litasoma namba ya gari, halafu unapotoka tutakuwa tumejua umetumia muda gani ukiwahi chini ya nusu saa tutakupiga faini,” amesema.
Amesema licha ya matangazo ya kuwataka madereva kuendesha mwendo wa spidi 50, lakini bado madereva hawazingatii.
Amesema baadhi ya watu wamelazimika kuyatelekeza magari yao hifadhini baada ya kuwagonga wanyama. Utaratibu ni kwamba kila mnyama mmoja ana bei yake na hivyo faini yake hutofautiana.  
“Leo hii ukimgonga tembo au twiga ni Dola 15,000 (zaidi ya Sh44 milioni), Dola 9,000 kama umemgonga faru (zaidi ya Sh26 milioni) hivyo nadhani ni muhimu kila mmoja wetu akijua athari za mwendo wa kasi hifadhini ili awe makini atakapopita hifadhini,”amesema.
Amesema Tanapa wataendelea kutoa elimu kwa wananchi kujua umuhimu wa hifadhi na faida yake kwa Taifa ili wawe sehemu ya kuhifadhi.
Naye Mhariri Martin Marela amesema kuwa anaamini elimu kwa wananchi na sheria bora zitasaidia kuongeza ushiriki wao katika uhifadhi.
Yusuph Katimba amesema wahariri wakielimishwa kwa kina kuhusu masuala ya uhifadhi na viumbe hai, watasaidia jamii kuelewa na hivyo kuleta mabadiliko.
Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Anita Mendoza amesema wanahabari wana jukumu kubwa la kuhakikisha rasilimali zilizopo zinatunzwa na kutumika kwa faida ya walio wengi.
“Tukiwa na uelewa wa kina wa uhifadhi na mgawanyo wa rasili