TAEC yafuatilia Wafanyakazi 2000 wanaofanya maeneo hatarishi ya mionzi
Muktasari:
- Tume ya Nguvu za Atomiki nchini Tanzania (TAEC) imesema imekuwa ikifuatilia kiwango cha mionzi kilichoko katika miili ya wafanyakazi 2,000 ambao wamekuwa wakifanya kazi katika maeneo ya mionzi.
Dodoma. Tume ya Nguvu za Atomiki nchini Tanzania (TAEC) imesema imekuwa ikifuatilia kiwango cha mionzi kilichoko katika miili ya wafanyakazi 2,000 ambao wamekuwa wakifanya kazi katika maeneo ya mionzi.
Akizungumza leo Jumamosi Agosti 14, 2021 Mtaalam wa Maabara wa tume hiyo Sarah Lema amesema kati ya idadi hiyo ni wafanyakazi 250 ndio wanafanya kazi katika maeneo hatarishi.
Lema ameyataja maeneo hatarishi ni yale yanayotoa tiba ya mionzi ikiwemo hospitali ya Ocean Road, Bugando na KCMC.
“Tunawapa kifaa kinachopima mionzi watu wanaofanya kazi katika maeneo yenye uhatarishi mkubwa kifaa hicho kinatakiwa kurejeshwa kila baada ya mwezi” amesema Lema.
Amesema watu wanaofanya kazi maeneo yasiyo na hatari kubwa kama vile migodini na sehemu za tafiti mbalimbali hurudisha kifaa hicho kila baada ya miezi mitatu.