Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Spika wa Bunge la Uganda afariki dunia

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

Spika wa Bunge la Uganda, Jacob Oulanyah amefariki dunia nchini Marekani alipokuwa anapatiwa matibabu.

Kampala. Spika wa Bunge la Uganda, Jacob Oulanyah amefariki dunia nchini Marekani alipokuwa anapatiwa matibabu.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ametangaza kifo cha spika huyo leo Jumapili Machi 20, 2022 kupitia akaunti yake ya Twitter.

Katika ujumbe wake aliotaangaza kifo hicho, Rais Mseveni amemtaja Oulanyah kama kada mzuri.

Hakuweka wazi kilichosababisha kifo cha Spika huyo ambaye alikuwa amelazwa hospitali nchini Marekani kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Oulanyah aliingia kwenye nafasi hiyo Mei 2021 na kabla ya kuwa Spika alikuwa naibu Spika kuanzia 2011.

Oulanyah mwanasheria na mwanasiasa wa muda mrefu aliwahi kuwa mbunge wa Kaunti ya Omoro, Kaskazini mwa Uganda.

Oulanyah alikuwa miongoni mwa wanasiasa kutoka eneo hilo walioshiriki katika mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Uganda na waasi wa Lord's Resistance Army walioongozwa na Joseph Kony miaka ya 2000.