Sheikh mteule Dar awaomba Watanzania kumuombea

Dar es Salaam. Sheikh mteule wa Mkoa wa Dar es Salaam,Walid  Alhad Omar ametoa ujumbe kwa waumini wote wadini hiyo na Watanzania kwa ujumla kumuombea dua kwa majukumu mapya aliyopewa.

Sheikh huyo ambaye ni Imamu Mkuu wa Msikiti wa Kichangani Magomeni, kwa sasa anakaimu nafasi hiyo wakati akisubiria kuapishwa kufuatia aliyekuwa akishika nafasi ya Sheikh wa Mkoa huo

Alhad Mussa Salum kutenguliwa jana Februari 2, 2023.

Uamuzi wa kutenguliwa Shekh Salum, ulifikiwa na jopo la Baraza la Ulamaa la Baraza Kuu la Kiislamu Tanzania (Bakwata) lililoketi kwa siku mbili jijini Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wake, Mufti Abubakar Zubeir.

Leo, Februari 03, 2023 Mwananchi lilitembelea majira ya 7:00 mchana kwenye Msikiti wa Kichangani wakati wa swala iliyoongozwa na Sheikh huyo mteule licha ya kuwataka waumini kudumisha amani kama dini hiyo inayotaka, lakini aliowaomba waumini kumuombea.

"Nimeteuliwa ni maamuzi na mapenzi ya Mungu kwa hiyo nawaomba waumini na Waislamu wote na Watanzania mniombee dua nikayafanye vyema majukumu mapya," amesema Sheikh huyo mteule.

Baada  ya kuisha swala hiyo ilikusanya waumini wengi kulikuwa na hafla maalumu ya kumpongeza kwa kupata uteuzi huo ambapo waumini wote walikuwa wanampa mkono ishara ya kumtakia majukumu mema.

Baada ya kuisha tukio hilo lilofanyika ndani ya msikiti, Sheikh huyo mteule alitoka nje ya msikiti kuwasalimia akina mama waliokuja kuswali na kupiga nao picha ya pamoja huku kina mama hao wakitoa maneno ya shukrani kwake.

Hata hivyo, Mwananchi ilipomfuata azungumzie uteuzi huo, Sheikh huyo mteule alisema "Siwezi kuzungumza Kwa sasa nasubiria niapishwe kwanza ndipo nitawaita na kuzungumza na kujibu maswali yenu yote," amesema Sheikh Walid.


Waumini watoa neno

Wakizungumza kwa nyakati tofauti waumini wa msikiti huo baada ya suala hiyo wamesema elimu aliyokuwa nao, busara na hekima zake anastahili kushika wadhifa huo na kutekeleza majukumu yake Kwa weledi.

Jamhuri Kihwelu aliyewai kuwa kocha wa Timu ya Taifa, Serengeti Boys, amesema kuteuliwa kwake siyo jambo lilozuka tu, ilipangwa na Mungu.

"Lakini amini aliyetoka hakuna mbaya isipokuwa Mungu aliona wakati wake wa kuondoka umefika na kuingia mwingine kwangu. Mimi Waislamu tumepata mtu mzuri wa kushika madaraka," amesema

Amesema ni mtu mzuri katika kutoa ushauri, msheshi na ni mkarimu wa kupenda watu kwenda kuswali kwenye msikiti wake na wamtakia mema asiwe na kiburi awaongoze Kwa busara Waislamu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Amis Rajabu Mzee wa Msikiti wa Kichangani amesema Sheikh huyo ni msikivu na anapenda kuwasilikiza wote lakini pia kiongozi mwenye dira za maendeleo.

"Tumeanza naye tangu umeanza huu msikiti, tuko naye amesimamia tumejenga msikiti huu pamoja na kujenga shule wanayosoma wanafunzi wetu ni mtu sahihi Kwa wana Dar es Salaam," amesema


xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx