Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sh80 milioni kuokoa maisha ya watoto wenye magonjwa ya moyo

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa takwimu, inakadiriwa kuwa watoto 1,500 nchini Tanzania hugundulika kila mwaka na matatizo ya moyo ya kuzaliwa.

Dar es Salaam. Katika juhudi za kuboresha afya na ustawi wa jamii nchini, Benki ya Stanbic Tanzania imetoa mchango wa Sh80 milioni kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Heart Team Africa Foundation. Mchango huu unalenga kusaidia watoto wanaokabiliwa na magonjwa ya moyo na mishipa ya damu, ambao wanahitaji matibabu ya kuokoa maisha.

Hafla ya kutangaza mchango huu ilifanyika katika Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam, ikihudhuriwa na mgeni rasmi Rais Mstaafu, Dk Jakaya Mrisho Kikwete. Hafla hii iliandaliwa na wadau mbalimbali kutoka sekta za umma na binafsi, wakikusanyika kwa lengo la kuchangisha fedha za kugharamia matibabu muhimu kwa watoto wanaohitaji msaada huu.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Stanbic Tanzania, Manzi Rwegasira, ameeleza dhamira ya benki hiyo katika kusaidia sekta ya afya kwa vitendo. “Tunajivunia kushiriki katika juhudi hizi muhimu za kusaidia watoto kupata matibabu ya kuokoa maisha. Mchango wetu ni sehemu ya kuunga mkono kazi kubwa inayofanywa na JKCI na Heart Team Africa Foundation kwa ajili ya jamii yetu,” alisema Rwegasira.

Kwa mujibu wa takwimu, inakadiriwa kuwa watoto 1,500 nchini Tanzania hugundulika kila mwaka na matatizo ya moyo ya kuzaliwa.

Gharama za matibabu huwa ni mzigo mkubwa kwa familia nyingi, ambao mara nyingi hawawezi kumudu wenyewe. Hivyo, JKCI na Heart Team Africa Foundation husaidia kwa kutoa ruzuku ya matibabu na kupunguza gharama kwa familia hizo.

Hata hivyo katika mpango huo wa kuchangisha fedha, inakadiriwa kuwa Sh4 milioni zinahitajika kwa ajili ya kumtibu mtoto mmoja.

Katika kufunga hafla hiyo, Rwegasira alitoa wito kwa wadau wa sekta zote kuunga mkono miradi inayotoa matumaini na msaada kwa watoto wa kesho.

“Pamoja, huruma na ukarimu wetu unaweza kuleta mabadiliko makubwa,” alisema, akionyesha dhamira ya Benki hiyo kuendelea kuwekeza katika sekta ya afya na kuimarisha jamii za Kitanzania.