Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sh692 bilioni zafyekwa mradi wa anuani za makazi

Rais Samia Suluhu Hassan akishuhudia Makamu wa Rais Dk Philip Mpango akipokea kwa niaba yake Bango lenye Anwani ya Makazi ya Ofisi ya Rais, Ikulu mara baada ya kuzungumza katika Kikao Kazi cha Wakuu wa Mikoa kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi. Picha na Ikulu

Muktasari:

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaonya wakuu wa mikoa kutotumia fedha za kugharamia mradi wa anwani za posta na makazi kwa ajili ya matumizi mengineyo (OC).

Dodoma. Rais Samia Suluhu Hassan amewaonya wakuu wa mikoa kutotumia fedha za kugharamia mradi wa anwani za posta na makazi kwa ajili ya matumizi ya mengineyo (OC).

 Pia, Mkuu huyo wa nchi amesema kuwa awali mradi huo ulipangwa kutumia Sh720 bilioni lakini gharama hizo zimepunguzwa hadi kufikia Sh28 bilioni.

Rais Samia amesema hayo leo Jumanne Februari 8, 2022 wakati akizungumza katika kikao kazi cha wakuu wa mikoa jijini hapa.

“Fedha tutaleta kwa ukubwa wa mikoa yenu pande zote (Tanzania Bara na Zanzibar), fedha hizi sio OC (matumizi mengineyo) ni ya mradi. Mtaendelea kutumia OC zenu, fedha iende katika miradi,”amesema.

Amesema halmashauri zinatakiwa kuchangia fedha katika utekelezaji wa mradi huo.

Ameshauri utekelezaji wa mradi huo kutumia nyenzo zilizopo katika kuukamilisha ili kufanikisha shughuli ya sensa ya watu na makazi ambayo itafanyika Agosti mwaka huu.

Rais Samia pia awaagiza viongozi kuwashirikisha watanzania kwa kuwafundisha kuhusu umuhimu wa mradi huo wa anwani za posta na makazi ili waweze kuwa na uelewa na kushiriki ipasavyo.

Amesema mradi huo utafanyika kwa utaratibu wa operesheni maalum kama ilivyofanyika katika ujenzi wa madarasa yaliyotokana na fedha za Uviko-19.

Amesema mradi huo unatakiwa kukamilika itakapofika Mei mwaka huu.

“Kama hamkumaliza zoezi au halikwenda vizuri tutakaa ana kwa ana, ukiwa na changamoto zake tuzungumze ukikaa nazo hadi muda ukamalizika itabidi tukae ana kwa ana tuelezane,”amesema.