Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sh137 milioni zatumika kujenga mochwari Msoga

Muktasari:

  • Wananchi wa eneo la Msoga na maendo jirani sasa wataondokana na kero ya kufuata huduma ya kuhifadhi miili ya ndugu zao katika hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo baada ya jengo la kuhufadhia maiti katika hospitali yao kuanza kujengwa.

Pwani. Zaidi ya Sh137 milioni zimetumika kujenga jengo la kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Msoga iliyopo Halmashauri ya Chalinze mkoani Pwani ambayo awali ilikuwa haina huduma hiyo.

Jengo hilo limejengwa kupitia utekelezaji wa miradi ya maendeleo unaofanywa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii uliochini ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (Tasaf) kwa kushirikiana na halmashauri mbalimbali nchini.

Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi wa jngo hilo leo Septemba 2023, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amesema utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini unalenga kuboresha huduma za kijamii kwa maeneo yenye uhitaji.

Kabla ya kujengwa kwa jengo hilo wananchi walilazimika kuifuata huduma hiyo katika hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo.

“Miradi hii ni kwa ajili ya maendeleo yetu sote, hivyo ni muhimu kwa wananchi kuendelea kujitolea kushiriki katika ujenzi wa miundombinu hii ambayo inajengwa na Tasaf katika maeneo yetu,” amesema.

Amesema Serikali imeridhishwa na viwango vya ujenzi wa jengo hilo kwa kile alichokieleza kuwa thamani ya fedha katika mradi imeonekana.

Oscar Maduhu ambaye ni Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf, amesema jengo hilo ni muhimu kwani litaboresha upatikanaji wa huduma za kibinadamu.

“Ujenzi wa jengo hili ni mradi ambao sisi wote ni wadau, huduma zinazotolewa zinatuhusu sisi sote, tunawasihi wasimamizi wa hospitali hii pamoja na mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze kuutunza ili uweze kuhudumia wananchi kwa muda mrefu,” amesema Maduhu na kuongeza;

“Niwahakikishie kuwa Tasaf bado ina fursa nyingi katika miradi ya miundombini, ni jukumu la halmashauri kuangalia uhitaji uliopo na kuleta maombi kwa ajili ya utekelezaji.”

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze, Ramadhan Possi alisema Sh4 bilioni zimefikishwa kwa walengwa 9,081 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/22 na 2022/23.

“Kupitia Tasaf, halmashauri yetu pia imetekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya ajira za muda kwa walengwa yenye jumla ya Sh440.8 milioni, miradi ya miundombinu yenye thamani ya Sh333.6 milioni huku walengwa wakiweza kuanzisha vikundi 322 vya kuweka na kukopa,” alisema Possi.