Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yapendekeza kuongeza kodi ya majengo, nyumba za nyasi hazihusiki

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba

Muktasari:

  • Serikali ya Tanzania imewasilisha Muswada wa Sheria ya Fedha mwaka 2023 na kupendekeza kuongeza kodi na kufuta kodi katika baadhi ya maeneo.

Dodoma. Serikali imependekeza kuongeza kodi ya majengo kutoka Sh12,000 hadi Sh18,000 kwa mwaka kwenye majengo yasiyo ya ghorofa.

  

Mapendekezo hayo yamewasilishwa leo Jumatatu Juni 26, 2023 na Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba wakati akiwasilisha Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2023.

Dk Mwigulu amependekeza kufanyiwa kwa marekebisho kwa Sheria ya Serikali za Mitaa ya Utozaji wa Kodi ya Majengo ili kuongeza kodi katika majengo ya ghorofa kutoka Sh60,000 kwenda Sh 90,000 kwa kila sakafu ya ghorofa.

“Lengo la hatua hii ni kuakisi kodi na thamani halisi ya majengo. Marekebisho yanafanyika katika kifungu hicho kwa kuwezesha asilimia 20 ya mapato kurejeshwa halmashauri ili kuziwezesha katika ufuatiliaji na ukusanyaji wa kodi hizo,”amesema.

Aidha, Dk Mwigulu amependekeza marekebisho ili kujumuisha maeneo yote ya wilaya katika utozaji wa kodi ya majengo isipokuwa majengo yaliyosamehewa katika Sheria.

Dk Mwigulu amesema lengo ni kuweka usawa katika kulipa kodi na pia wanapendekeza marekebisho ya sheria ili kuongeza maeneo ambayo hayatahusishwa na utozaji wa kodi ya majengo.

Ameyataja maeneo hayo kuwa ni pamoja na nyumba za tope, fito, tembe, nyasi na nyumba zinazofanana na hizo kwa ajili ya makazi.

Aidha, amependekeza marekebisho kwenye Sheria ya Mifumo ya Malipo ya Taifa, ili kufuta tozo ya miamala kwenye kila muamala wa kutuma fedha na badala yake kubakiza tozo kwenye miamala ya kielekroniki ya kutoa fedha.

“Lengo la marekebisho haya ni kuondoa utozaji wa tozo ya muamala mara mbili kwenye miamala mmoja pamoja na kuchochea ufanyaji wa miamala kwa njia za kielektroniki (cashless transactions),”amesema.