Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali kumuenzi Hayati Magufuli kwa kusimamia uwajibikaji

Waumini wakiwa katika ibada ya kumbukumbu ya kumwombea Hayati Magufuli iliyofanyika leo Machi 17, 2024 katika Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Yohana Maria wa Muzeyi.

Muktasari:

Biteko amesema Serikali inaendelea kumkumbuka Magufuli sio tu kama Rais wa Tanzania bali kama kiongozi aliyeweka misingi ambayo Serikali awamu ya sita inaendelea kutekeleza

Geita. Serikali imesema itaendelea kuyaenzi yote yaliyofanywa na Rais hayati John Magufuli kwa kusimamia uwajibikaji kwa kuondoa uzembe, kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.

Akizungumza katika ibada ya kumbukumbu ya kumwombea Hayati Magufuli iliyofanyika leo Machi 17, 2024 katika Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Yohana Maria wa Muzeyi, Naibu Waziri Mkuu, Doto Biteko amesema kila kilichobuniwa na Magufuli, Serikali ya inakiendeleza kwa kasi ikiwa ni njia ya kumuenzi kwa vitendo.

Biteko amesema Serikali inaendelea kumkumbuka Magufuli sio tu kama Rais wa Tanzania bali kama kiongozi aliyeweka misingi ambayo Serikali awamu ya sita inaendelea kutekeleza.

“Miradi mbalimba ambayo Magufuli aliibuni kama ujenzi wa Bwawa la Julius Nyerere, Rais Samia amesukumwa na ujenzi ule, umefika mwisho, Magufuli alikuwa na ndoto ya kuwaunganisha Watanzania kwa reli ya kisasa, Rais Samia ameendeleza ndoto hiyo na ujenzi wa kipande cha reli kutoka Dar es salaam majaribio yamefanyika.

“Kwa watu wa kanda ya ziwa mikoa ya Geita na Mwanza ilikuwa inamkera sana kuchukua muda mrefu kwenye kivuko cha Busisi na akaamua uanzishwe ujenzi wa daraja ambalo sasa limefika zaidi ya asilimia 80, Rais aliposema kazi iendelee, alikusudia kuendeleza maono aliyokuwa,” amesema Biteko.

Katika hatua nyingine, amemshukuru mke wa Rais Magufuli, Janeth Magufuli ambaye kwa sasa anamuuguza mama mkwe na wifi zake kwa kuendelea kusiamamia umoja wa familia.

Akizungumza kwenye ibada hiyo, mtoto wa hayati Magufuli, Jesca Magufuli amesema leo, ikiwa ni miaka mitatu tangu kifo cha baba yao, kimekuwa kipindi kigumu sana kwao kama watoto.

Amesema kwa niaba ya watoto wote, anamshukuru Rais Samia kwa kuwashika mkono tangu walipoondokewa na baba yao na kusema amekuwa akiwasaidia kwa kutatua changamoto zozote zinazowakabili.

“Kwa niaba ya wenzangu, tunapenda kumshukuru mama yetu, Janeth Magufuli kwa kuendelea kuisimamia vema familia huku akibeba majukumu ya ubaba na yale yake kama mama wa familia, haikuwa rahisi lakini kwa neema ya Mwenyezi Mungu umeyaweza yote kwa yeye atutiaye nguvu,” amesema Jesca.

Akimzungumzia Magufuli, amesema alikuwa mume mwema na baba bora pamoja na kiongozi mwema wa nchi yake na wataendelea kumuenzi na kumkumbuka kwa namna alivyowalea na kuwawekea misingi mizuri ya kuchapa kazi na kumtanguliza Mungu mbele.

Shigela alivyofanya kazi na JPM

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela akizungumza kwenye ibada hiyo, amesema wakati wa uhai wake Rais Magufuli alikuwa akipenda kupiga simu saa tisa usiku na walikuwa wakilazimika kukaa kusubiri.

Amesema ilikuwa  ikifika saa nne hulali, unakaa unasikilizia ukiona hajapiga hadi saa 11, unaamua kulala na yeye saa 11:30 alfajiri ndiyo anapiga, ukikuta amekupigia ukiwa hujapokea, unaanza kujiuliza mara mbilimbili hii siku itaisha au haitaisha.

Amesema Rais Magufuli alikuwa mtu mwenye upendo na watumishi wake na kumpongeza mama Janeth kwa kuendelea kujenga umoja na mshikamano kwenye familia.

Amesema Rais Samia ameendelea kusimamia misingi iliyoanzishwa na Rais Magufuli akitolea mfano Hospitali ya Kanda ya Chato ambayo wakati wa kifo chake ilikuwa haijaanza kutoa huduma lakini sasa inatoa huduma za kibingwa.

Amesema Rais Samia amekamilisha ndoto ya Rais Magufuli kwa kujenga jengo kubwa lenye uwezo wa kubeba vitanda 300 linalojengwa kwa thamani ya Sh14 bilioni ambalo ujenzi wake umefika asilimia 90 kwa sasa.

Kwenye miundombinu ya barabara Rais Magufuli alikuwa na ndoto ya kuunganisha Barabara ya Kahama –Geita ambayo sasa ujenzi wa barabara ya Kahama –Kakola yenye urefu wa kilomita 60 tayari wamesaini na mkandarasi amekabidhiwa kazi kwa ajili ya kuanza ujenzi huku ujenzi kipande cha Kakola - Geita kikitarajiwa kuanza wakati wowote mwaka huu.