Sarafu Za Kidijitali Ni Nini? - Jinsi Blockchain Inavyoenea Duniani

Muktasari:
- Teknolojia hii imetikisa tasnia zote ulimwenguni kwa sababu imeongeza ufanisi katika fedha
- Teknolojia ya Blockchain na kazi yake duniani
- Mali za kidijitali chini ya mtandao wa Blockchain
- Faida za mali za kidijitali
- Kazi ya Kampuni ya Yellow Card hapa Tanzania
Na Hezron Nkanda. Dunia ya kidijitali inakua kwa kasi ya kipekee. Kuna wajanja wapya ambao wameunda maeneo mapya kwenye wavuti ambayo hayajawahi kuskika, hadi sasa wanaendelea kulisukuma gurudumu la kidijitali pembezoni mwa wavuti pasipofikirika.
Tukiwa tunaongelea juu ya suala la dijitali, huwezi kuacha kutaja teknolojia ya blockchain. Teknolojia hii imetikisa tasnia zote ulimwenguni kwa sababu imeongeza ufanisi katika fedha.
Ilianza na Bitcoin mnamo 2009 ikisaidiwa na Blockchain; mfumo wa kurekodi shughuli za kidijitali. Blockchain ni aina maalum ya hifadhi taarifa ambapo habari anuwai zinaweza kuhifadhiwa. Matumizi ya kawaida hadi sasa imekuwa kama kitabu cha shughuli zinazotokea mtandaoni.
Moja wapo ya hizo shughuli ni matumizi ya mali za kidijitali maarufu kama Cryptocurrency, ama Digital Assets.
Mali ya dijiti ndio ya kwanza kati ya mambo mengi ya blockchain ambayo watu wanatumia hivi sasa. Mali za kidijitali zina shikilia thamani. Mali hizi zinaweza kuhifadhiwa au kubadilishwa kwenye mifumo ya kompyuta, haswa kwenye wavuti.

Tofauti kati ya mali za kidijitali na uhifadhi wa fedha kwenye benki, ni kwamba benki zinaweka riba kubwa hadi 15%. Mali za dijiti hazikugharimu. Licha ya hivyo, malipo kupitia benki huchukua muda mrefu. Ambapo, kwenye mali za kidijitali, malipo hufanyika ndani ya dakika chache.
Ndani ya mali za kidijitali kuna sarafu mbalimbali kama Bitcoin, Ethereum, Tether na kadhalika. Mali za kidijitali zinaweza tumika kununua, kutunza na kubadilishana na mali zingine.
Fedha zetu zinapungua thamani kila mwaka kutokana na mfumuko wa bei. Lakini ukiwa na mali za kidijitali, mali hiyo haina mfumuko wa bei. Thamani ya mali za kidijitali hupanda kutokana na uhitaji, na sio kitu kingine.
Mali hizi pia husaidia watu kutunza thamani. Na kama uliwahi kununua Bitcoin mwaka 2009, basi thamani yake ya Bitcoin ulizonunua zitakuwa zimepanda kwa asilimia 20,000,000% hadi sasa. Hata ukitaka kufafanua zaidi kwenye mtandao wa Google ni mali ipi inayopanda kwa kasi duniani, jibu litakuja: Bitcoin.
Mali ambazo tayari zipo katika fomu ya dijiti kwenye mtandao wa Blockchain zina usalama zaidi, maana Blockchain inatumia teknolojia tata inayohakikisha kwamba hakuna mtu anayeweza kuingia kwenye akaunti yako na kuchukua mali zako (kama hajui nywila yako).

Mtandao wa Blockchain unarekodi taarifa kupitia kompyuta zaidi ya 3,800,000 (milioni tatu na laki nane) ambazo zimesambazwa duniani nzima. Kwahiyo kama mtu akijaribu kubadilisha taarifa kwa kutumia kompyuta moja, taarifa haziwezi badilika, kutokana na hizo taarifa kusambazwa papo hapo na mfumo wa Blockchain.
Hivi sasa, kuna nchi chache ambazo zimeanza kutumia mali za kidijitali kwa mfano, El Salvador imekuwa nchi ya kwanza ulimwenguni kuainisha rasmi Bitcoin kama mali halali ya thamani. Rais wa El Salvador Nayib Bukele alisema kuwa uhalalishaji wa Bitcoin na mali zingine za dijiti "kutaleta ujumuishaji wa kifedha, uwekezaji, utalii, uvumbuzi na maendeleo ya uchumi nchini kwetu".
Miaka ijayo tunapoelekea, tunaweza kutarajia benki kuu za ulimwengu kuanza kuunda sarafu zao za kidijitali. Mnamo Aprili, Benki ya Uingereza ilitangaza kuwa wako katika mchakato wa kuanzisha sarafu ya benki kuu ya dijiti.

Nchini Tanzania, YellowCard imekuja kwa dhoruba. Yellow Card ni kampuni ya ubadilishaji wa mali za dijiti inayotokea Marekani. Kampuni ya Yellow Card imekuja barani Afrika kwajili ya kuwezesha watu wapate nafasi ya kupata mali za kidijitali.
Kampuni ya Yellow Card inawawezesha watu kununua, kuuza na kuhifadhi mali za kidijitali. Yellow Card ni kampuni ya fintech inayokua kwa kasi zaidi, na sasa imeanzisha uwepo wake katika nchi 9 barani Africa na ina mipango ya kuongeza hatua zake hivi karibuni.
Kampuni ya Yellow Card imekuja Tanzania kuelimisha jamii kuhusu mali za kidijitali. Kwa wale ambao wangependa kujua zaidi kuhusu mfumo wa Blockchain pamoja na mali zake za kidijitali, tembelea tovuti ya: academy.yellowcard.io. Kama una nia ya kumiliki mali yako ya kwanza ya kidijitali, huduma ya Yellow Card inapatikana kwenye kivinjari cha wavuti yellowcard.io/Tanzania na kupitia programu za android na iOS chini ya jina la ‘Yellow Card’. Kwa sasa, huduma ya Yellow Card inaambatana na VisaCard, MasterCard na Mobile Money. Huduma hiyo imefunguliwa rasmi kwa soko la Tanzania.
Lakini kabla ya kumiliki mali yako ya kwanza ya kidijitali, unashauriwa utembelee tovuti ya Yellow Card Academy ili upate kujifunza mlolongo mzima wa mali za kidijitali. Ni muhumi kupata elimu kwanza kabla ya kuwekeza.