Samia, Mwinyi na Kinana wapita kwa kishindo

Mshindi wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM, Abdulrahman Kinana upande wa Bara (kushoto) Rais wa Zanizbar, Dk Hussein Mwinyi akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti kwa upande wa Zanzibar wakijadiliana jambo jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi
Muktasari:
- Uchaguzi huo umefanyika leo Jumatano Disemba 7, 2022 Jijini Dodoma, ambapo viongozi hao walikuwa wakigombea nafasi hizo peke yao.
Dar es Salaam. Msimamizi wa uchaguzi wa CCM, Dk Ali Mohamed Shein amemtangaza, Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa mara nyingine baada ya kupigiwa kura za ndio 1914 kati 1915.
Uchaguzi huo umefanyika leo Jumatano Disemba 7, 2022 Jijini Dodoma, ambapo viongozi hao walikuwa wakigombea nafasi hizo peke yao.
Mbali na hao, Dk Shein ambaye ni Rais mstaafu wa Zanzibar, amemtangaza pia Abdulrahman Kinana kuwa Makamu mwenyekiti wa CCM, Bara baada ya kutetea nafasi hiyo baada ya kupigiwa kura za ndio 1913 kati ya 1915.
Pia amemtangaza Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Zanzibar, baada ya kupigiwa kura za ndio 1912.