Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RC Homera aagiza waliohusika kufyeka mahindi kusakwa, kulipa fidia

Mbeya. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amekemea vikali kitendo cha mtu, watu waliovamia shamba lenye ukubwa wa nusu heka na  kufyeka mahindi ya  wananchi  katika eneo la wazi linalokodishwa na Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (Tazara) Kata ya Iyunga jijini hapa.

 Homera ametoa kauli hiyo leo, Jumatano Februari 8, 2023 baada ya kuona taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha wananchi wanalalamikia kufyekwa kwa mazao yao usiku wa kuamkia leo  Jumatano Februari 7 mwaka huu.

“Kama Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan haitaweza kuvumilia kitendo kama hicho hata kama walikiuka sharia, ikiwepo maeneo hayo kutoruhusiwa kulima kwa sababu ya kudhibiti matukio ya uharifu na ujangili,”amesema.

Amesema kitendo hicho kimesababisha taharuki na kuleta njaa katika familia huku akitahadharisha wenyeviti wa Serikali za mitaani, watendaji wakati wa kukemea na kuzuia wananchi kutopanda mazao ilikuwa mwezi  Desemba mwaka jana kabla hawajalima na kutumia gharama kubwa za mbolea, mbegu na vibarua wa kulima.

Amesema kiuhalisia mtu hata kama kuna changamoto zozote zinazojitokeza kwenye jamii uwezi kuchukua jukumu la kuingia kwenye mashamba yanayotegemewa kwa chakula na kuanza kufyeka badala ya kutumia busara wavune mazao ndio wapige marufuku.

“Tayari nimemtuma Mkuu wa Wilaya, Beno Malisa afike eneo la tukio kufanya tathmini ya idadi ya watu waliothirika, ikiwemo waliohusika kufyeka ili wawajibike kulipa fidia haraka iwezekanavyo kwani eneo hilo lilikuwa ni mali ya Tazara ambao wanatoa vibali kwa wananchi,” amesema.


Kwa upande wake

Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Dourmohamed Issa alisema tangu baraza la madiwani lililopita lilitoa azimio kwamba hapa mjini hakutakiwi kulimwa mazao ambayo yanazidi inchi moja.

"Hii ni kwa sababu ya kuzuia uharifu maeneo ambayo maficho ya watoto 'magangwe' ambao wanafanya uharifu ikiwemo kuvuta bangi hivyo tuliona tuepuke nalo na tulishatoa agizo hilo," alisema Issa.

Mkazi wa Iyunga, Fidea Saimon amesema kuwa kitendo kilichofanywa siyo cha kiungwana na kuunga mkono agizo la Mkuu wa Mkoa wananchi walioathirika kulipwa fidia.