Rais Samia mgeni rasmi mkutano wa wakutubi, masekretari

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejinenti ya Utumishi wa Umma, George Simbachawene
Muktasari:
- Kwa mara ya kwanza mkutano wa Makatibu Muhtasi na Watunza kumbukumbu utafanyika Visiwani Zanzibar kuanzia Mei 22 hadi 27.
Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa Makatibu Muhtasi na Watunza kumbukumbu Mei 22 Visiwani Zanzibar.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumanne, Mei 16, 2023 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejinenti ya Utumishi wa Umma, George Simbachawene amesema kwa mara ya kwanza mkutano huo utafanyika Visiwani Zanzibar kuanzia Mei 22 hadi 27 mwaka huu.
Simbachawene amesema maandalizi kwa ajili ya kikao hicho yamekamilika ambapo zaidi ya wageni 8000 wanatarajia kuhudhuria.
"Nichukue nafasi hii kuwaomba waajiri wote ambako wanachama wa vyama hivi viwili wapo kuwahudumia kwa kila kitu," amesema Simbachawene.
Amesema hayo yalikuwa ni maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha anaufanya Utumishi wa Umma unakuwa uliotukuka na unawahudumia wananchi.