Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia ateua viongozi Necta, UDSM

Muktasari:

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya viongozi wawili ndani ya Baraza la Taifa la Mitihani (Necta) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi wawili akiwemo Profesa William Anangisye kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Mitihani (Necta).

 Profesa Anangisye ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anaendelea na wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya cha awali kukamilika.

Taarifa iliyotokewa leo Alhamisi Agosti 25, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imesema pamoja na Profesa Anangisye, Balozi Mwanaidi Maajar ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza wa UDSM.

Balozi Maajar anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji mstaafu, Damian Lubuva aliyemaliza muda wake. Jaji Luvuba amewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Uteuzi huo umeanza leo Alhamisi Agosti 25, 2022.