Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia ataka wadau kuchangamkia mkutano AGRF

Muktasari:

  • Ikiwa zimebaki siku chache kabla ya kufanyika kwa Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika 2023 (AGRF), Rais Samia Suluhu Hassan, amewaita wadau kushiriki mkutano huo.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan, amewaita wadau wa ndani na nje kujisajili ili waweze kushiriki katika Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika 2023 (AGRF), unaotarajiwa kufanyika Septemba 5 hadi 8, 2023.

Mkutano huo wa siku tatu unatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam.

Rais ametoa wito huo alipotembelea banda la AGRF lililopo katika maonyesho ya Nanenane yaliyoanza Agosti 1 mwaka huu jijini Mbeya katika Viwanja vya John Mwakangale.

Akizungumza na Wananchi, Rais Samia amesema Tanzania imepata fursa ya kuandaa mkutano huo mkubwa hivyo ni vyema kujiandaa ipasavyo.

"Niwaombe watanzania, kampuni za nje zilizopo Tanzania kujiandikisha na kushiriki katika mkutano huu," amesema Samia.

Amesema nchi za Afrika na nyingine kutoka bara la Afrika zitakaa na kujadili namna ya kujitosheleza kwa chakula na kuangalia mfumo wa chakula ndani ya bara la Afrika.

Mkutano huo unafanyika nchini ikiwa tayari Tanzania inatekelezwa ajenda ya 10/30 ambayo inalenga kuongeza mchango wa kilimo katika pato la Taifa.

"Katika hili Serikali Imekuja na programu ya kushirikisha vijana na wanawake katika sekta ya kilimo ambayo inahususha ufugaji, uvuvi na kilimo cha mazao kupitia mradi wa BBT (Jenga Kesho Iliyobora),"

Rais yuko mkoani Mbeya kwa ajili ya kuhitimisha maonyesho ya wakulima maarufu Nanenane ambayo yamefanyika kwa mwaka wa pili mfululizo.