Rais Samia amteua Katibu Mtendaji Necta

Muktasari:
- Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dk Said Mohammed kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta).
Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dk Said Mohammed kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta).
Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, uteuzi huo umeanza leo Februari 27, 2023.
Kabla ya uteuzi, Dk Mohammed alikuwa ni Mkurugenzi wa Huduma za Ufundishaji, Mafunzo na Mitihani, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).