Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NBC yakabidhi Kombe la Ubingwa wa Vijana (U20) kwa Azam FC

Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Biashara  Benki ya NBC ambae ndio Mwenyekiti wa kamati ya Ligi Kuu ya NBC ndani ya benki hiyo, Bw Joseph Lyuba (alievaa fulana nyeupe) akikabidhi kombe la Ligi ya NBC ya Vijana chini ya miaka 20 (NBC U20 Youth League) kwa nahodha wa timu ya Azam FC (U20) Ismaily Ally baada ya timu hiyo kuwa bingwa wa ligi hiyo kwa msimu wa 2024/2025.

Dar es Salaam. Mdhamini mkuu wa Ligi ya  NBC Vijana chini ya miaka 20 (NBC U20 Youth League) Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imekabidhi kombe la ubingwa wa ligi hiyo kwa timu ya Azam FC (U20) ya jijini la Dar es Salaam baada ya timu hiyo kuibuka bingwa wa ligi hiyo kwa msimu wa 2024/2025 kufuatia ushindi wake wa goli 1 – 0 dhidi ya wenzao Foutain Gate  (U20).

Shujaa wa Azam FC  (U20) jana alikuwa ni mshambuliaji Carlos Chasambi aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 11 ya mchezo.

Hafla ya kukabidhi kombe la ubingwa huo ilifanyika  jana katika uwanja wa Chamazi Complex  jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Biashara benki ya NBC ambae ndio Mwenyekiti wa kamati ya Ligi Kuu ya NBC ndani ya benki hiyo, Joseph Lyuba aliwaongoza wafanyakazi wengine wa benki hiyo kwenye tukio hilo lililopambwa na uwepo wa mashabiki na wadau mbalimbali wa mchezo huo wakiongozwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, Katibu Mkuu wa TFF,  Wilfred Kidao  na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoani Dar es Salaam (DRFA), Lameck Nyambaya.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Lyuba alivipongeza vilabu shiriki vya ligi hiyo hususani mshindi timu ya Azam FC (U 20), mshindi wa pili Fountain Gate  FC (U20), mabenchi ya ufundi pamoja na TFF huku akielezea namna ambavyo ushindani kwenye ligi hiyo umeboreka, hatua ambayo kwa mujibu wake inathibitisha muelekeo mzuri katika ukuaji wa mchezo wa soka hapa nchini.

Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Biashara  Benki ya NBC ambae ndio Mwenyekiti wa kamati ya Ligi Kuu ya NBC ndani ya benki hiyo, Bw Joseph Lyuba (wa pili kulia) sambamba na  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia (alievaa kofia), Katibu Mkuu wa TFF,  Wilfred Kidao  na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoani Dar es Salaam (DRFA), Lameck Nyambaya (kulia) wakiongoza zoezi la uvalishaji wa medali kwa wachezaji wa timu ya Azam FC (U20) baada ya timu hiyo kuwa bingwa wa Ligi ya NBC ya Vijana chini ya miaka 20 (NBC U20 Youth League) msimu wa 2024/25

“Msukumo wa NBC kudhamini ligi hii ya vijana unachagizwa na dhamira yetu ya kuwa na ligi kuu yenye ubora na ushindani kutokana na vipaji vinavyozalishwa hapa nchini. Tunaamini ili tuwe na Ligi Kuu ya NBC yenye mvuto na ushindani lazima tuanzie katika ngazi hii ya kuibua vipaji. Tunashuru kuona hili linaenda vizuri na matunda yake yataonekana zaidi kwenye ligi za NBC Championship, ligi Kuu ya NBC na hata timu ya Taifa,’’ alisema Lyuba.

Kwa mujibu wa Lyuba, Benki hiyo imejipanga zaidi kuendelea kuboresha udhamini wake kwenye ligi zote tatu inazozidhamini ili kuongeza kasi ya ushindani, kuboresha hadhi ya ligi hiyo, kuchochea ajira pamoja na kuboresha hali ya maisha ya wadau mbalimbali waliopo kwenye mnyororo wa mchezo huo ikiwemo wachezaji na mabenchi ya ufundi.

Akizungumzia mashindano hayo, Kocha Mkuu wa Azam FC (U20), Kassim Liogope pamoja na kuwapongeza wachezaji wake, uongozi wa timu hiyo, TFF na mdhamini benki ya NBC, alisema mashindano hayo yaliambatana na ushindani mkubwa  hususani katika hatua ya nane bora kutokana na timu shiriki kubadilika kiuchezaji  hatua ambayo inathibitisha uborekaji mkubwa wa viwango vya ubora wa vilabu vinavyoshiriki ligi hiyo.