Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mzumbe kumtunuku Rais Samia udaktari wa heshima

Leo Jumapili, Novemba 2 4, 2024 ni mahafali ya 23 ya Chuo Kikuu cha Mzumbe, Mkoa wa Morogoro.

Katika mahafali hayo yatakayofanyikia chuoni hapo, 
Rais wa  Tanzania, Samia Suluhu Hassan atatunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima katika Uongozi ya Chuo Kikuu Mzumbe.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa William Mwegoha amesema hiyo itakuwa  shahada  ya kwanza ya heshima kutolewa na chuo hicho tangu kuanzishwa kwake.

Shahada hiyo ya udaktari wa heshima itakuwa ya tano  Rais Samia kuoewa tangu alipoingia madarakani Machi 19, 2021 akichukua kijiti cha mtangulizi wake, hayati  John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021.

Shahada nyingine nne ametunukiwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Tanzania), Chuo Kikuu cha Zanzibar, Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru (India) na Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki.

Aidha, Profesa Mwegoha amesema suala la usawa wa kijinsia limepiga hatua chuoni hapo akitolea mfano, wahitimu wa mwaka huu,"ni karibu 50/50 kwani asilimia 50.2 ya wahitimu ni wanaume na asilimia 49.7 ni wanawake. Naweza kuona jinsi tunavyopiga hatua kwa vitendo."