Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwili wa mwanafunzi IFM aliyekatwa kichwa wawasili Moshi, kuzikwa leo

Mwili wa mwanafunzi James Temba (24) aliyeuawa kwa kukatwa shingo na mwili wake kukutwa unaelea katika Mto Msimbazi, jiijini Dar es Salaam James Temba ukiwa umewasili leo Alhamisi Mei 7, 2026 katika Kijiji cha Mande, Kata ya Old Moshi Magharibi, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Muktasari:

  • Mwanafunzi huyo wa mwaka wa kwanza katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), James Temba (24) aliondoka nyumbani kwao Aprili 29 mwaka huu na hakurudi na baadaye mwili wake kukutwa katika Mto Msimbazi, jijini Dar es Salaam, ukielea ndani  ya maji, huku ukiwa umekatwa kichwa.

Moshi. Mwili wa mwanafunzi James Temba (24) aliyeuawa kwa kukatwa shingo na mwili wake kukutwa unaelea katika Mto Msimbazi, jiijini Dar es Salaam James Temba umewasili leo Alhamisi Mei 7, 2026 katika Kijiji cha Mande, Kata ya Old Moshi Magharibi, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya maziko.

Mwili huo ambao utazikwa bila kichwa katika makaburi ya familia nyumbani hapo, ulipowasili umeingizwa moja kwa moja ndani kama ilivyo taratibu za Wachaga na kisha familia kufanya ibada fupi.

Baada ya taratibu za familia kukamilika na mchungaji kufika nyumbani hapo  mwili huo utatolewa nje kwa ajili ya kutoa fursa ya ndugu jamaa na marafiki kuuaga mwili huo ambao utazikwa baadaye katika eneo la makaburi ya familia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na  mwongozaji wa shughuli hiyo ya mazishi, Ramso Msoka amesema kutokana na hali ya hewa familia na mchungaji wamekubaliana kufanya ibada ya mazishi nyumbani hapo tofauti na ilivyokuwa awali kwamba mwili huo ungeagwa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mande.

Mwili wa mwanafunzi James Temba (24) aliyeuawa kwa kukatwa shingo na mwili wake kukutwa unaelea katika Mto Msimbazi, jiijini Dar es Salaam James Temba ukiwa umewasili leo Alhamisi Mei 7, 2026 katika Kijiji cha Mande, Kata ya Old Moshi Magharibi, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

"Kutokana na mazungumzo yaliyofanyika kati ya mchungaji na familia  ya Temba, ibada ya mazishi itafanyika nyumbani hapa kutokana na changamoto ya hali ya hewa," amesema Ramso.

Temba, aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), aliondoka nyumbani kwao Aprili 29 mwaka huu na baadaye mwili wake kukutwa katika Mto Msimbazi, jijini Dar es Salaam, ukielea ndani ya maji, huku ukiwa umekatwa kichwa.

Mwili wa mwanafunzi James Temba (24) aliyeuawa kwa kukatwa shingo na mwili wake kukutwa unaelea katika Mto Msimbazi, jiijini Dar es Salaam James Temba ukiwa umewasili leo Alhamisi Mei 7, 2026 katika Kijiji cha Mande, Kata ya Old Moshi Magharibi, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mei 3 mwaka huu, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam lilithibitisha kifo cha Temba na kueleza kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha kifo hicho, na watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi.