Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwabukusi: Sitishwi kunyang’anywa vyeti

Wakili Boniface Mwabukusi

Muktasari:

  • Baada ya Kamati ya Mawakili kumshtaki Wakili Boniface Mwabukusi kwa madai ya kumkosea Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wakili huyo amesema atayajibu mashtaka hayo na kuwa haogopi kufutiwa vyeti vyake vya kitaaluma

Arusha. Baada ya Kamati ya Mawakili kumshtaki Wakili Boniface Mwabukusi kwa madai ya kumkosea Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wakili huyo amesema atayajibu mashtaka hayo na kuwa haogopi kufutiwa vyeti vyake vya kitaaluma.

Barua hiyo, ambayo Mwananchi imeiona iliyosainiwa na Katibu wa kamati hiyo, Faraji R. Ngukah, ilitumwa Julai 14 na kupokelewa na Mwabukusi Julai 31, 2023 imemtuhumu Mwabukusi kwa kutoa maneno ya kashfa dhidi ya viongozi wa Serikali, Bunge na mfumo wa utoaji haki.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Arusha, wakili huyo alisema atajibu hoja hizo ipasavyo.
"Nimeona malalamiko ya AG dhidi yangu, mimi niseme tu, kwanza siogopi na wala sibabaishwi kwa sababu mimi siishi kwenye vyeti, sikuzaliwa kuwa wakili.”

“Mimi ni Mtanganyika haki yangu ya utanganyika haiwezi kuzuiwa au kuwa controlled (kudhibitiwa) kupitia vyeti vya kitaaluma au vitisho, mimi siyo mtu wa kutishwa," amesema.

Amesema wakati anaanza kupinga mkataba wa makubaliano ya uwekezaji wa bandari kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai, alijiandaa kisheria kwa lengo la kulinda rasilimali za kizazi cha sasa na baadaye.

"Madai yale yamesukumwa na msimamo wangu kuhusua suala la bandari na ninataka niwahakikishie, kama msimamo huu umewatisha hii ni rasharasha, sasa tunakwenda kudondosha mvua ya masika,” amesema na kuongeza;

"Hatutababaika, hatutatetereka na nitazijibu hoja ipasavyo, labda hoja ambayo siwezi kuijibu ni hii, ombi lake la mimi kufutiwa vyeti, hilo naweza nikamkubalia vifutwe vyote mpaka vya darasa la saba. Mungu aliniumba jinsi nilivyo, iwe ni vyeti, mali, vyote tunavikuta hapa tutaviacha,” amesema.

Wakili huyo aliendelea kusisitiza kuwa hakuna mtu anayeweza kumpangia kuhusu masuala ya ulinzi wa Taifa lake, kwani ni wajibu binafsi na hawezi kuruhusu bandari itolewe kwa mkataba wa kizembe.

"Akili siyo cheti, wengi wamesoma lakini hawana akili, mimi nina akili zangu timamu. Kama ni kufungua mashauri nitafungua vizuri tu na kama ni kuhamasisha Watanznaia nitahamasisha kwa nguvu zaidi na ari zaidi bila hofu, vyeti kwangu naona ni karatasi zinazonionyesha nimekaa darasani muda gani, lakini kunisaidia kufanya chochote sijaona na nimeanza kupambania haki yangu tangu zamani," amesema.