Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mvua ya upepo yabomoa makazi, yaua kikongwe Nyang’wale

Jengo la choo cha shule ya msingi Lubando Wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita lililoezuliwa kwa upepo mkali ulioambatana na mvua iliyonyesha Oktoba 15, 2023.

Muktasari:

Oktoba 6, 2023 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitaoa tahadhari ya uwezekano wa mvua za El Nino katika maeneo kadhaa nchini ikiwemo mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Geita. Mvua iliyoambatana na upepo imesababisha kifo cha mzee Mathias Nkomera (79) pamoja na kuezua paa za wakazi wa Wilaya ya Nyang’hwale mkoani.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu leo Oktoba 17, 2023, Katibu Tawala Wilaya ya Nyang’wale, Kaunga Amani amesema mvua hizo zimenyesha Oktoba 15, 2023.

Katibu Tawala huyo aliyezungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale, Grace Kingalame amesema madhara zaidi yameripotiwa katika tarafa za Nyang’hwale na Nyijundu.

‘’Nyumba zilizoathirika zaidi ni zenye ukuta wa udongo na kuezekwa kwa mabati,’’ amesema Kaunga

Amesema pamoja na makazi ya watu, madhara ya mvua hizo pia zimeonekana katika taasisi za elimu ikiwemo shule ya Sekondari Busolwa ambako miti imeangukia paa za madarasa mawili na kuharibu mfumo wa umeme.

Rebeca Mathias, mjukuu wa mzee Mthias aliyepoteza maisha katika janga hilo amesema babu yake amefariki kwa kuangukiwa na ukuta wa nyumba uliobomoka.

“Mvua ilianza Saa 12:00 jioni; ndugu wengine walikuwa kwenye nyumba moja huku babu akiwa kwenye nyumba nyingi, ghafla tuliona mabati ya paa la nyumba alimokwemo babu yakiezuliwa na kurushwa mbali na upepo na ukuta kumwangukia babu,’’ amesema Rebeca

Diwani wa Kata ya Shabaka, Karim Chasama amesema zaidi ya nyumba 100 zimeathirika kwenye kata hiyo na kuiomba Serikali na wadau wengine kuwasaidia waathirika ambao baadhi licha ya kukosa makazi, pia wamepoteza akiba yote ya chakula iliyoharibiwa kwa maji ya mvua.

Ofisa Mtendaji Kijiji cha Lubando, Mtika John amesema uongozi wa Serikali ya kijiji unaendelea kufanya tathmini kubaini madhara halisi ya mvua hizo.

Oktoba 6, 2023 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitaoa tahadhari ya uwezekano wa mvua za El Nino katika maeneo kadhaa nchini ikiwemo mikoa ya Kanda ya Ziwa.