Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Musoma Vijijini yakabiliwa na upungufu wa madawati zaidi ya 12,000

Musoma Vijijini yakabiliwa na upungufu wa madawati zaidi ya 12,000

Muktasari:

  • Halmashauri ya wilaya ya Musoma vijijini mkoani Mara inakabiliwa na upungufu wa madawati 12,054 kwa shule za msingi hali ambayo inasababisha baadhi ya wanafunzi kukaa chini wawapo darasani.

Musoma. Halmashauri ya wilaya ya Musoma vijijini mkoani Mara inakabiliwa na upungufu wa madawati 12,054 kwa shule za msingi hali ambayo inasababisha baadhi ya wanafunzi kukaa chini wawapo darasani.

Kaimu Afisa elimu msingi katika halmashauri hiyo, Baraka Maingu amesema kuwa halmashauri hiyo ina jumla ya madawati 11,830 kati ya madawati 23, 884 yanayohitajika.

Akizungumza leo Oktoba 5,2021 wakati wa kupokea msada wa madawati 100 yaliyotolewa na benki ya NMB kwa shule ya Msingi Kiriba, Maingu amesema kuwa jitihada mbalimbali zinafanyika ili kumaliza changamoto hiyo ikiwa ni pamoja na kushirikisha wadau ili wanafunzi wote 71,653 waweze kukaa kwenye madawati.

"Pia tunatumia fedha zinazotolewa na serikali kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa madarasa mfano mradi wa EP4R kwahiyo kwenye kuezeka tunatengeneza na madawati kwa kushirikiana na jamii, na pia tunapasua miti ya mbao iliyopo kwenye shule zetu tunatengeneza madawati" amesema.

Akikabidhi madawati hayo, mtunza fedha mkuu wa NMB, Aziz Chacha amesema kuwa madawati hayo 100 yana thamani ya zaidi ya Sh10 milioni na kwamba msaada huo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya huduma kwa mteja maadhimisho ambayo yanatarajiwa kusherehekewa na benki hiyo kwa muda wote wa mwezi huu.

Amesema kuwa ndani ya mwezi huu wa Oktoba benki hiyo inatarajia kufanya shughuli kadhaa katika jamii ambapo shughuli hizo ni pamoja na utoaji wa udhamini kwa wanafunzi 50 wanaotoka katika familia duni kwaajili ya kujiunga na elimu ya vyuo vikuu nchini.

"Kabla mwezi huu kuisha tutatangaza ' Scholarship' kwa wanafunzi 50 waliofanya vizuri kwenye mitihani yao ya kidato cha sita lakini wanatoka katika familia masikini kwahiyo tunataka na wao pia wapate nafasi ya kujiunga na vyuo vikuuu ili watimize ndoto na malengo yao ya elimu," amesema.

Amesema kuwa mbali na wanafunzi hao lakini pia benki hiyo nwakani itatangaza ufadhili kwa wanafunzi 150 kujiunga na elimu ya kidato cha tano hasa kwa wale watakaofanya vizuri lakini wakiwa wanatoka katika familia zenye hali duni kimapato.

Amesema kuwa hayo na miongoni mwa malengo ambayo benki hiyo imejiwekea katika kurudisha shukrani kwa jamii kutokana na ukweli kuwa jamii imesaidia kwa kiwango kikubwa benki hiyo kuwa benki kubwa zaidi nchini.


Akipokea msadaa huo, katibu tawala wa wilaya ya Musoma, Justine Manko amesema kuwa moja ya sera ya serikali ni ushirikiano baina yake na sekta binafsi ili kuleta ustawi wa jamii katika kuboresha huduma ndani ya jamii.



Amesema kuwa serikali inalenga kuboresha huduma za kijamii lakini ushirikiano kuyika sekta binafsi unahitajika ili kugikia lengo hilo na kuomba wadau wengine kuiga mfano huo wa NMB ili kuwa na maendeleo endelevu nchini.

Mwisho


Summary

Benki ya NMB imetoa msaada wa madawati 100 yenye thamani ya zaidi ya Sh10 milioni kwa shule ya Msingi Kiriba iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Musoma vijijini msaada ambao unalenga katika kupunguza changamoto ya madawati katika shule za msingi kwenye halmashauri hiyo.