Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtuhumiwa adaiwa kujiua kwa kujinyonga akiwa mahabusu

Muktasari:

  • Awali alikuwa akituhumiwa kufanya tukio la mauaji ya baba yake mzazi Novemba 22, 2025 kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali shingoni na alitoroka hadi alipokamatwa kwa tukio la kamshambulia na kumdhuru baba yake mdogo.
     

Moshi. Mkazi wa Mtaa wa Karikacha, Kata ya Rau, mkoani Kilimanjaro, Michael Lambau (18) anadaiwa kujiua kwa kujinyonga akiwa mahabusu ya Kituo cha Polisi Moshi kati alikokuwa akishikiliwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo jana Januari 13, 2026.

Aidha, Kamanda Maigwa amesema awali mtuhumiwa huyo alikamatwa Januari 13, 2026 kwa kosa la kumshambulia na kumpiga kwa bapa la panga baba mdogo wake aitwaye Brian Felix.

"Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linafanya uchunguzi wa tukio la kujiua kwa mtu mmoja aitwaye Michael Lambau (18), mkazi wa Mtaa wa Karikacha, Kata ya Rau Manispaa ya Moshi akiwa mahabusu katika kituo cha Polisi Moshi Kati alikokuwa akishikiliwa kwa kosa la shambulio la kudhuru mwili,"amesema Kamanda Maigwa

Amefafanua,  mtuhumiwa alikamatwa Januari 13, 2026 kwa tuhuma za kumshambulia kwa kumpiga na mabapa ya panga Brian Felix ambaye ni baba yake mdogo.

Pamoja na mambo mengine, Kamanda Maigwa amesema awali alikuwa akituhumiwa kufanya tukio la mauaji ya baba yake mzazi Novemba 22, 2025 kwa kumchoma kitu chenye ncha kali shingoni, na alitoroka hadi alipokamatwa kwa tukio hilo la shambulio la kudhuru mwili.



Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi.