Mtoto miaka 11 adaiwa kujinyoga Lindi

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa taarifa hiyo ilieleza kuwa mtoto huyo alijinyonga kwa kutumia nguo ambapo sababu ya kufanya hivyo haijajulikana. 

Lindi. Jeshi la Polisi Mkoani Lindi limetoa taarifa ya kujinyonga hadi kufa kwa mtoto Yusra Hassan Ally (11) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili kutoka kata ya Nyengedi, Halmashauri ya Mtama, mkoani Lindi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ilieleza kuwa mtoto huyo alijinyonga kwa kutumia nguo ambapo sababu ya kufanya hivyo haijajulikana. 

Akizungumza na Waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi Alhaj Kabaleke Salim Hassan alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 17 majira ya saa Nane mchana.

Kabaleke alisema kuwa binti huyo alikuwa anaishi na bibi yake, ambapo siku hiyo ya tarehe 17 alishindwa kwenda shule kwa kisingizio kuwa anaumwa lakini alibakia akifanya usafi ikiwa ni pamoja na kufua nguo na kazi nyingine za nyumbani. 

Uchunguzi wa jeshi la Polisi ulibaini kuwa sababu ya kifo chake ni kujinyonga.

Nae Mwenyekiti wa kijiji cha Nyengedi A, Omari Baisa amesema kuwa mtoto huyo kwa muda mrefu alikuwa akiishi na babu yake upande wa baba kisha kuhamia nyumbani kwa bibi yake ambapo aliambiwa alinde mpunga.

Ambapo bibi huyo alienda sokoni kutafuta kitoweo baada ya yule bibi kutoka mtoto huyo alichukua maamuzi ya kuchukua nguo (kitenge pamoja na ndoo na kuzunguka nyuma ya nyumba na kujinyonga.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti, mtoto huyo alihamia kwa bibi yake akitokea kwa Babu yake  ambapo siku iliyofuata walienda shambani kuvuna mpunga na walipofika nyumbani waliuanika ambapo bibi yake alimuomba Yusra aangalizie mpunga usiliwe na kuku  na baadaye kumkuta akiwa amejinyonga.