Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtoto afa maji baharini Lindi

Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu Nuhu Shabani.

Muktasari:

  • Mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Msinjahili iliyopo Manispaa ya Lindi, Nuhu Shabani (9) amefariki dunia baharini.

Lindi. Mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Msinjahili iliyopo Manispaa ya Lindi, Nuhu Shabani (9) amefariki dunia baada ya kuzama kwenye Bahari ya Hindi akiwa anaogelea.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Aprili 9, 2024, alitoka nyumbani saa 12 jioni  akasema anaelekea msikitini mama mlezi wa marehemu, Sophia Hamisi amesema Nuhu alikuwa na tabia ya kurudi usiku saa 4 au 5 lakini jana.

Sophia amesimulia kuwa baada ya kukaa hadi saa 5 usiku bila kurudi, ilibidi waanze kumtafuta maeneo mbalimbali bila mafanikio yoyote, ikabidi watoe taarifa polisi, ndipo alipotolewa nguo za watoto wawili, wakamwambia aangalie hizo nguo kama kuna ya mtoto wake.

Sophia anaendelea kueleza kuwa baada ya kuonyeshwa nguo za mtoto wake, wakamwambia kuwa mwenye nguo hii amefariki dunia na mwili wake umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Sokoine.

“Nuhu alikuwa ana kawaida ya kurudi nyumbani usiku, sasa mimi na baba yake tulipoona hadi saa 5 usiku hajarudi, tukasema tusihangaike kumtafuta kwa kuwa ndio kawaida yake kurudi usiku, ilipofika saa 5 hajarudi ikabidi mume wangu aende kituo cha polisi kutoa taarifa.

“Alipofika kule wakamtolea nguo za watoto wawili, wakamwambia atazame nguo ya mwanae, alipoitazama na kuigundua, wakamwambia ameshafariki na mwili upo hospitali ya Sokoine,” amesema Sophia.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine, Dk Alexander Makalla amekiri kupokea mwili huo saa 1:50 usiku wa jana.

Jirani wa marehemu, Zuhura Mohamedi amesema wazazi wanatakiwa watambue watoto wao wapo wapi muda wote, wasiwaache kwenda baharini wenyewe, kama wanaenda basi waende na mtu mzima wa kuwaangalia.

“Sasa hivi dunia imeharibika, kuna vitendo vya kikatili vinaendelea kila wakati, mtoto unatakiwa umchunge wewe mwenyewe mzazi, sio kumuacha peke yake, niwaombe wazazi wezangu tuwalinde watoto wetu hasa kipindi hiki mvua zinanyesha sana mkoani kwetu,” amesema Zuhura.

Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Lindi, Joseph Mwasabije amesema walipogiwa simu majira ya saa 12 jioni kuna mtoto amezama baharini, walitoka eneo la Sea View na kuupata mwili huo saa 7 usiku.

“Nitoe wito kwa wazazi na walezi kuwa makini na watoto hasa kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha, msiwaache watoto peke yao kama anaenda ufukweni inabidi uende naye, sio kumuacha mwenyewe,” amesema Kamanda Mwasabije.