Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwalimu afa ndani ya tanki la maji

Mwalimu afa ndani ya tanki la maji

Muktasari:

Mwalimu wa Shule ya Msingi Michungwani wilayani Handeni, Athumani Nondo amekutwa amefariki akiwa ndani ya tenki la maji lililokuwa nje ya nyumba yake baada ya kutafutwa kwa siku mbili mfululizo.

Handeni. Mwalimu wa Shule ya Msingi Michungwani wilayani Handeni, Athumani Nondo amekutwa amefariki akiwa ndani ya tenki la maji lililokuwa nje ya nyumba yake baada ya kutafutwa kwa siku mbili mfululizo.

Akielezea mkasa huo, diwani wa Kata ya Segera, Onesmo Makomero alisema taarifa walizopata ni kwamba Jumanne iliyopita marehemu aliondoka saa 2:30 usiku na familia yake haikujua alikoenda hivyo ikaanza kumtafuta bila mafanikio na Ijumaa mchana mwili wake ndani ya tanki.

“Mwili wa marehemu umekutwa Ijumaa majira ya saa saba mchana ndani ya Simtank lililopo nje ya nyumba yake,” alisema Onesmo.

Rafiki wa marehemu, Hassan Chambago alisema baada ya kumtafuta bila mafanikio “juzi, Ijumaa ilibidi tufanye dua maalum kumwombea maana ni muumini mwenzetu, baada ya dua tunatoka msikitini tukapewa taarifa kwamba marehemu amepatikana ndani ya tanki la maji,” alisema Chambago.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga, Blasius Chatanda amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema wanaendelea kuchunguza.