Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mradi wa umeme Rusumo kuzinduliwa Februari, 2025

Muonekano wa nje wa mradi huo wa umeme wa maporomoko ya maji Rusumo wilayani Ngara mpakani mwa Tanzania, Rwanda na Burundi

Muktasari:

  • Mradi wa umeme wa maporomoko ya maji Rusumo unazalisha megawati 80 nakuzisambaza kwa nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi, ambapo kila moja inapata megawati 27.

Ngara. Baada wa uzinduzi wa mradi wa umeme Rusumo utakaonufaisha nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi kuwa kimya kwa zaidi ya mwaka, Mawaziri wanaohusika na nishati kutoka nchi hizo wamekubaliana kuzindua mradi huo Februari 2025.

Mradi huo ulioanza kujenga 2017 kwa gharama ya zaidi ya Sh850 bilioni fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia (WB) na kutakiwa kuzinduliwa Machi, 2023 kwa sasa umefikia asilimia 99.9, utazalisha umeme wa megawati 80 huku kila nchi ikinufaika kwa megawati 27.

Leo Novemba 15, 2024 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko amekutana na Waziri wa Miundombinu wa Rwanda, Gasore Jimmy pamoja na Waziri wa Nishati na Madini wa Burundi, Ibrahim Uwizeye  kuzungumzia mustakabali wa mradi huo uliopo katika maporomoko ya Mto Rusumo Wilaya ya Ngara mkoani Kagera.

Akizungumza baada ya kikao na mawaziri hao, Dk Biteko amesema kilichokuwa kinakwamisha uzinduzi wa mradi huo ni viongozi (Marais) wa nchi hizo kutopata muda kwa wakati mmoja wakuweza kuudhulia uzinduzi huo.

"Leo tumekutana tena na kujadiliana tena tukaona mradi uzinduliwe Februari,2025 na tumekubaliana wote kwa pamoja mawaziri wa nchi hizi tupeleke ombi kwa viongozi wetu wa juu kuweza kuudhuria kwa pamoja," ameeleza Dk Biteko

Naye, Waziri wa Miundombinu nchini Rwanda, Gasore Jimmy amesema mpaka sasa nchi ya  Rwanda inazidi kufaidika baada ya mradi huo kukamilika na kuanza kutumika maana umeongeza kipato cha nchi na kusaidia kuboresha miundombinu ya maendeleo.

"Tunafurahi kuona mradi mzuri tunawashukuru Benki Kuu na nchi zetu kuwa na umoja mzuri wananchi wetu na serikali tunazidi kunufaika, tunatumia umeme huu na leo tumekubaliana iwezekane tuzindue mradi huu,"

Waziri wa Nishati na Madini nchini Burundi, Ibrahim Uwizeye amesema ni vizuri wanapoona mradi unaendelea vizuri, ujenzi umekamilika na kuwanuafaisha kama nchi tatu moja za Afrika Mashariki, kuungana na kutumia umeme unaozalishwa kupitia mradi wa maporomoko ya maji Rusumo.

Mkuu wa Mkoa Kagera,Fatma Mwassa akieleza kuwa baada ya mradi huo kukamilika kwa asilimia hizo wananchi wa wilaya ya Ngara wameanza kuchangamkia fursa za kiuchumi kwa kuanzisha viwanda vidogo vodogo ambavyo vimesaidia kuchangia miundombinu na  pato la taifa kupitia kodi wanazolipa.