Mpina awasili mbele ya kamati ya maadili CCM

Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina akiwasili katika Kamati ya Maadili ya CCM Wilaya ya Meatu. Picha na mpigapicha wetu
Simiyu. Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina ameitikia wito wa Ofisi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Meatu, mkoani Simiyu iliyomtaka afike leo, Alhamisi 2024 kwa ajili ya mahojiano ya masuala mbalimbali.
Mpina aliyewahi kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi amewasili mchana wa leo Alhamisi, Januari 25, 2024 kwa ajili ya kuhojiwa na Kamati ya Usalama na Maadili ya wilaya hiyo.
Jana Jumatano, Katibu wa CCM Wilaya ya Meatu, Joel Makwaia aliiambia Mwananchi Digital kuwa wamemwita Mpina mbele ya kamati hiyo kutokana na mambo mbalimbali yaliyojitokeza.