Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Moto wateketeza mabweni Shule ya Sekondari Bigwa Sisters Moro

Mabweni ya Shule ya Sekondari ya Bigwa Sisters iliyopo Manispaa ya Morogoro yakiteketea kwa moto jana jioni wakati wanafunzi wakiwa kwenye ibada kanisani. Picha Hamida Shariff

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati moto huo unatokea wanafunzi na walimu walikuwa wakifanya ibada kwenye kanisa lililomo ndani ya shule hiyo

Morogoro. Moto uliozuka ghafla katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Bigwa Sisters  umeteketeza mabweni matatu na mali za wanafunzi zikiwamo nguo, madaftari na vifaa vingine vya kujifunzia.

Tukio hilo limetokea jana jioni Jumapili, Julai 26, 2026 wakati wanafunzi na walimu wao ambao ni watawa wa kike wakifanya katika ibada kanisa lililomo ndani ya shule hiyo.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro, Shabani Marugujo amesema taarifa za kuzuka kwa moto huo zilipokewa ofisini kwake saa 11:38 jioni.

Amesema kikosi cha askari kilifika katika shule hiyo na kukuta tayari moto umeshashika kasi.

"Tulipofika eneo la tukio tuliwakuta wananchi, wanafunzi na watawa wakiendelea na jitihada za kuuzima moto huo kwa kutumia maji yaliyokuwa kwenye ndoo na mchanga, hivyo tuliungana nao na kuanza kuzima kwa kutumia maji kutoka kwenye mitambo yetu," amesema Kamanda Marugujo.

Mabweni ya Shule ya Sekondari ya Bigwa Sisters iliyopo Manispaa ya Morogoro yakiteketea kwa moto jana jioni wakati wanafunzi wakiwa kwenye ibada kanisani. Picha Hamida Shariff

"Baada ya muda mfupi Incharge wa kikosi,  Stafu Sajenti Alexander Makulun aliomba mitambo mingine ya kuzima moto ifike kwa ajili ya kuongeza nguvu, kwa kuwa moto huo ulikuwa bado ni mkubwa na baada ya saa kadhaa ulizimwa wote."

Kamanda Marugujo amesema hakuna vifo wala majeruhi waliotokana na tukio hilo na kwamba mpaka sasa chanzo cha moto huo bado hakijafahamika na wanaendelea na uchunguzi.

Kiongozi wa kikosi cha askari waliofanya kazi ya kuzima moto huo, Alexander Makuluni ametaja baadhi ya mali zilizoteketea kwa moto ni vifaa vya kujifunzia wanafunzi yakiwamo madaftari, baadhi ya magodoro, nguo, shuka, mabegi na vitu vingine mbalimbali.

Mkuu wa shule hiyo, Sista Esta Mkwizu amesema tukio hilo limewashtua na hafahamu chanzo cha moto huo.

"Uongozi wa shule tumepokea kwa masikitiko makubwa tukio hili na kwa sasa siwezi kusema ni hasara kiasi gani tumepata kwa sababu ndio kwanza kumekucha na tunaendelea kuangalia hii hasara, nadhani baadaye nitaweza kuzungumza vitu vilivyonyooka na vyenye uhakika," amesema Sista Mkwizu.