Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Morogoro yataja vipaumbele mwaka wa fedha 2022/23

Meya wa Manispaa ya Morogoro Pascal Kichanga akizungumza wakati wa mkutano wa kawaida wa baraza la madiwani. Picha na Lilian Lucas.

Muktasari:

  • Wakati Manispaa ya Morogoro ikijiwekea malengo ya kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, inatarajia kukusanya Sh86.7 bilioni katika mwaka wa fedha 2022/23.

Morogoro. Wakati Manispaa ya Morogoro ikijiwekea malengo ya kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, inatarajia kukusanya Sh86.7 bilioni katika mwaka wa fedha 2022/23.

Hayo yamebainishwa na leo Jumanne Julai 19,2022 na Meya wa Manispaa ya Morogoro, Pascal Kihanga wakati wa mkutano wa kawaida wa mwaka wa baraza la madiwani la Manispaa ya hiyo.

Kichanga amesema kuwa Sh12.6 bilioni zitatokana na mapato ya ndani, mishahara ni 64.4 bilioni, Matumizi mengineyo ni Sh1.1 bilioni na miradi ya maendeleo ni Sh8.5 bilioni.

Ametaja vipaumbele sita vya manispaa hiyo kuwa ni pamoja na makusanyo ya mapato, elimu, afya, usafi wa mji na utunzaji wa mazingira, utawala bora na mipango miji.

Amesema kupitia fedha hizo pia watamalizia miradi ambayo bado haijakamilika ikiwemo ujenzi wa kituo cha Afya Tungi, kumaliza miundombinu ya zahanati ya Mji mkuu, Kauzeni, Mafiga na Kihonda sambamba na kumalizia majengo 50 ya madarasa ya shule za msingi.

Kihanga amesema Halmashauri hiyo imepanga kupima viwanja 12,000 katika shamba la Tungi Sisal Estate kwenye eneo la ukubwa wa hekta 4,500 katika kata ya Kihonda na Kata Mkundi katika mwaka huo wa fedha.

Hata hivyo, meya huyo amesema kuwa mwaka wa fedha 2021/22 Manispaa ilifanikiwa kukusanya Sh 65.9 bilioni ambayo ni sawa na asilimia 83.4 ya makadirio ya makusanyo ya Sh74.6 bilioni.

Akizungumza kwenye kikao hicho, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Morogoro, Chifu Sylvester Yaredi amewataka madiwani kufanya kazi kwa ushirikiano ili kutimiza malengo na ilani ya chama kama inavyokusudiwa ili kuwaletea wananchi maendeleo na kuufanya mkoa kupiga hatua ya kuwa Jiji.

Katika mkutano huo Diwani wa kata ya Sabasaba Mohamed Lukwele alichaguliwa kuwa Naibu Meya wa Manispaa hiyo kwa mara nyingine ambapo alipata kura 38 lililokuwa na madiwani 38 ambapo ataongoza katika kipindi cha mwaka mmoja 2022/23.