Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mganga wa jadi jela miaka 7 kuua bila kukusudia

Morogoro. Mahakama Kuu Kanda ya Morogoro imemhukumu kifungo cha miaka saba jela, Jumanne Ngasa (28) baada ya kumkuta na hatia ya kumuua bila kukusudia Christina John, mkazi wa Mafisa mkoani hapa.

Jaji wa Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro, Messe Chaba alitoa adhabu hiyo Septemba 1, 2023 baada ya kusikiliza na kuzingatia maelezo ya pande zote za kesi hiyo na kutoa hukumu.

Katika shauri hilo la mauaji namba 9 la mwaka 2023, Mahakama imetoa adhabu hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 198 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

Jaji Chaba alisema mshtakiwa alidaiwa kutenda kosa hilo Mei 24 mwaka 2020 katika maeneo ya Mafisa mkoani morogoro,

Shitaka hilo la mauaji ilitajwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo Machi 16, 2023 na mshtakiwa alikana.

Awali ilidaiwa kuwa, Mei 24, 2020 mshtakiwa alifika nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya kumpatia tiba ya asili akiwa kama mganga wa kienyeji na mara baada ya hapo mshtakiwa pamoja na marehemu, walitoweka na baadaye mshtakiwa alikamatwa katika stendi ya mabasi mkoani Tabora akiwa na sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zinazodaiwa zilikuwa za mume wa marehemu.

Lakini ilipofika Agosti 29, 2023 katika Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Morogoro, wakili wa mshtakiwa aliiomba Mahakama kuwa mshtakiwa wake ameonyesha nia ya kukiri kosa, lakini pia ameomba kubadilishiwa kosa kubwa kwenda kosa dogo kwa maana kosa la kuua kwa kukusudia na kwenda kwenye kosa la kuua bila kukusudia.

Kutokana na ombi hilo, Mahakama iliridhia na kubadilisha kosa hilo na hati ya mashtaka ilibadilishwa kutoka kwenye kuua kwa kukusudia na kwenda kwenye kuua bila kukusudia.

Akizungumza baada ya hukumu hiyo, Wakili upande wa utetezi Jovit Byalugaba alisema uamuzi wa mahakama umezingatia misingi ya haki, kwa sababu Jaji ameeleza kuwa mahakama lazima izingatie si haki tu kutendeka haki bali ionekane kwamba kweli haki imetendeka.

Hadi hukumu hiyo inatolewa, mshatakiwa Jumanne alikuwa tayari amekaa mahabusu takribani miaka mitatu.