Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mfanyabiashara kizimbani kwa kujipatia fedha kwa udanganyifu

Muktasari:

  • Mfanyabiashara, Kelvin Masero Kichonge (43) amefikishwa Mahakamani kwa kosa la kujipatia Sh106 milioni kwa njia ya udanganyifu, na matumizi ya fedha hizo ilikuwa kwa ajili ya kununulia mahindi.

Dar es Salaam. Mfanyabiashara, Kelvin Masero Kichonge (43) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kiasi cha Sh106 milioni.

Mshtakiwa huyo alisomewa mashitaka yake na wakili wa Serikali Mwandamizi Grace Mwanga   mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Ferdnadri Kihwonde.

Alidai kati ya Julai  hadi Novemba 2021 jijini Dar es salaam mshtkiwa akiwa na nia  ya kudanganya alijipatia kiasi cha sh106 milioni kutoka kwa  Zoran Popov kwa lengo la kununua na kuuza mahindi lakini  hakufanya hivo jambo ambalo alijua kuwa ni kinyume Cha sheria.

Baada ya kusomewa mashtaka yanayomkabili alikana kutenda kosa hilo na upelelezi umekamilka.

Hakimu Kihwonde amesema dhamana ipo wazi kwa mshtakiwa huyo, hivyo wanatakiwa wadhamini wawili wanaotambulika kisheria ambao watawasilisha fedha taslimu Sh53 milioni au mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh53 milioni.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 9, 2023 kwa ajili ya kumsomea mshitakiwa hoja za awali.