Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mchengerwa asisitiza makandarasi wazawa kutonyimwa tenda

Waziri wa Nchi Ofisi ya Dais Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa (kulia) akikabidhi kitendea kazi kwa Mtendaji Mkuu wa Tarura nchini, Mhandisi Victor Seff mara baada ya kuzindua Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Barabara za mijini na vijijini (Tarura). Picha na Hawa Mathias

Muktasari:

  • Ameiagiza Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (Tarura) kufuata sheria na kanuni zilizopitishwa na Wizara ya Fedha ili kuhakikisha tenda zinatolewa kwa kampuni za makandarasi wazawa.

Mbeya. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa ameeleza kutoridhishwa na hali ya makandarasi wazawa kukosa tenda za ujenzi wa miradi ya barabara kwa kisingizio cha ukosefu wa mitaji.

Kutokana na hilo, Mchengerwa ameiagiza Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (Tarura) kufuata sheria na kanuni zilizopitishwa na Wizara ya Fedha ili kuhakikisha tenda zinatolewa kwa kampuni za makandarasi wazawa.

Akizungumza jana usiku, Jumamosi Julai 27, 2024, katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya Tarura iliyofanyika katika Hoteli ya Beaco, Mchengerwa amesema, "sipendezwi kabisa kuona makandarasi wazawa wanakosa tenda za miradi kwa visingizio vya mitaji. Ufike wakati wajengewe uwezo kama mataifa mengine yanavyofanya ikiwamo kuwapatia elimu, mitaji na nyenzo ili wapige hatua."

Amesema kwa kufanya hivyo, imesaidia fedha za miradi zitawanufaisha wao binafsi na kampuni zao, lakini pia Serikali kutokana na kodi watakazolipa.

Hata hivyo amesema suala la mtaji kwa makandarasi wazawa litakwisha baada ya kupitisha sheria ya hati fungani, aliyosema watamuomba Rais Samia Suluhu Hassan aizindue hivi karibuni.

Mchengerwa amesema bajeti ya Sh1.3 trilioni ya Tarura ikibaki kwa makandarasi wazawa itanufaisha familia nyingi.

Amesisitiza kuwa miradi ya chini ya Sh50 bilioni inapaswa kutolewa kwa makandarasi wazawa ili kukuza uchumi wa ndani.

Katika maagizo yake, Mchengerwa amesema hatarajii kusikia tena kuwa mameneja wanawanyima makandarasi wazawa kazi huku wageni wakipewa kipaumbele.

Amesema dhamana ya mitaji itatolewa na benki ili kusaidia makandarasi hao wazawa kushinda tenda hizo.

Awashukia watendaji Tarura

Wakati huohuo; Waziri Mchengerwa amewakemea baadhi ya watendaji wa Tarura  wanaoshindwa kushiriki vikao muhimu kwa kutuma wawakilishi na kuonya kuwa wizara sasa itaanza kulishughulikia suala hilo.

“Hii haikubaliki, sasa tutaanza kuchukuliana hatua, hatutaki watendaji muwe mnachukulia mambo kirahisi rahisi halafu tukae kimya,” amesema waziri huyo.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera aliishukuru Serikali kwa kuipatia Tarura fedha na kuanza kutekeleza miradi mingi kwa vitendo. Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Tarura, Victor Seff amemuahidi Mchengerwa kuwa miradi yote itatekelezwa kwa viwango na kipaumbele kitatolewa kwa makandarasi wazawa kama alivyoshauri.

Awali, Waziri Mchengerwa alishuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa stendi ya kisasa ya mabasi ya mikoani inayojengwa eneo la Old Airport na soko la kisasa la Matola.

Mkataba huo ulisainiwa baina ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya na Kampuni ya Sihotech Engineering Contractors Limited na AMJ Mult Contractors Company Limited JV, wenye thamani ya Sh30.1 bilioni.