Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbunge wa zamani wa Moshi Mjini afariki dunia

John Mwanga, aliyewahi kuwa Mbunge wa Moshi mjini.

Moshi. Aliyewahi kuwa Mbunge wa Moshi Mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), John Mwanga (78), amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, Machi 5, 2025.

Mwanga, ambaye alikuwa mbunge wa kwanza Moshi mjini  ulipoanza mfumo wa vyama vingi nchini, amefariki katika Hospitali ya Selian, mkoani Arusha, alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mtoto wa marehemu, Fortunate Mwanga, amethibitisha kifo cha baba yake akisema alikuwa anaugua kwa muda mrefu.
"Ni kweli baba yetu amefariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Selian, ambapo alikuwa amelazwa baada ya kuugua kwa muda mrefu," amesema Fortunate.

Amesema taratibu za mazishi zinaendelea na zitafanyika mkoani Arusha, Dar es Salaam na nyumbani kwake, Usharika wa Neema, KCMC, mkoani Kilimanjaro.


Endelea kufuatilia Mwananchi.