Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbunge ataka Sh27, 000 kuunganishiwa umeme

Muktasari:

  • Mbunge wa Iramba Mashariki (CCM), Fransic Mtinga ametaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuweka gharama za kuunganisha umeme kwa Sh27, 000 kote nchini ili kukusanya makusanyo mengi kutokana na mauzo ya umeme na kodi ya majengo.

Dodoma. Mbunge wa Iramba Mashariki (CCM), Fransic Mtinga ametaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuweka gharama za kuunganisha umeme kwa Sh27, 000 kote nchini ili kukusanya makusanyo mengi kutokana na mauzo ya umeme na kodi ya majengo.

 Ameyasema hayo leo Jumatano Mei 31, 2023 wakati akichangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2023/24.

Amesema Tanesco inafanya biashara kwenye kuuza umeme na kuunganisha umeme kwasababu wanatoza Sh320, 000 kwa maunganisho ya umeme mijini.

Amesema wanaounganisha umeme kwa kiasi hicho mijini, ni ndogo na kwamba wakati gharama zilipokuwa Sh27, 000 wateja walikuwa ni wengi sana.

“Kipindi ambacho ilitangazwa umeme uwekwe kwa Sh27000 maombi ya kuunganishiwa umeme yalijaa Tanesco hadi wakashindwa kufanya kazi lakini watu hawa ni wa mjini,”amesema.

Amesema watu wa mjini wana matumizi makubwa ya umeme na hivyo anaona fursa hiyo wameiacha ya kukusanya mapato mengi.

Mtinga amesema bora wangeweka Sh 27,000 kama gharama ya maunganisho kwa watu wote lakini baada ya muda mfupi watu wengi wakatumia umeme.

Amesema hatua hiyo itawafanya Tanesco kuingiza mapato kwasababu watu wa mjini wana matumizi makubwa ya umeme.

“Kama tunaweza kupeleka umeme zaidi ya kilometa 200 toka kijiji kimoja hadi kingine kwa gharama za Serikali na kwamba wataunganisha kaya 15 hadi 20. Kuna maeneo ambayo nguzo moja inaweza kubeba hadi mita 15,” amesema.

Amesema kwa Sh27, 000 zitawawezesha watu wengi kuanganisha umeme na Tanesco ikapata fedha kutokana na ununuzi wa umeme kuliko kuwawekea Sh320, 000 halafu hawavuti umeme.

Amesema kwanini wasitumie fursa kwa kukusanya kodi ya majengo ya Sh12, 000 kwa mwezi kila mita na kwamba wanaweza kuongeza mapato ya Serikali.