Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbulu yatumia Sh204 bilioni kwa maendeleo

Mkuu wa wilaya ya Mbulu mkoani Manyara, Michael Semindu akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa CCM mwaka 2020-2025 kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya CCM ya wilaya hiyo ambapo Serikali imetumia Sh204 bilioni kwa miradi mbalimbali ya maendeleo. Picha na Joseph Lyimo

Muktasari:

  • Fedha hizo zimetumika kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya elimu, afya na maji kwa mwaka 2020-2025.

Mbulu. Wilaya ya Mbulu imetumia Sh204 bilioni kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya elimu, afya na maji, katika kipindi cha miaka minne ya utawala wa Serikali ya awamu ya sita.

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara, Michael Semindu, ameyasema hayo leo Aprili 5, 2025 wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2020-2025 kwa wajumbe wa halmashauri kuu ya chama ya wilaya hiyo.

Semindu amesema kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan miradi mbalimbali ya maendeleo imenufaisha jamii.

Amesema kwenye elimu ya msingi walipatiwa Sh15 bilioni, elimu ya sekondari Sh22.7 bilioni na upande wa suala la lishe, afya na ustawi wa jamii walipatiwa Sh6 bilioni.

Semindu amesema kwenye kilimo, mifugo na uvuvi walipatiwa Sh8 bilioni na mpango wa kuhudumia kaya masikini (Tasaf) walipatiwa Sh8 bilioni.

"Kwenye miradi ya maji mamlaka ya maji na usafi wa mazingira vijijini (Ruwasa) imepatiwa Sh54 bilioni na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mbulu (Mbuwasa) imepatiwa Sh1 bilioni," amesema Semindu.

Amesema wakala wa barabara nchini (Tanroads) wilaya ya Mbulu imepatiwa Sh11 bilioni wakala wa barabara za mjini na vijijini (Tarura) Mbulu imepatiwa Sh23 bilioni, shirika la ugavi wa nishati ya umeme (Tanesco) Sh35 bilioni na mamlaka ya mapato (TRA) Mbulu imekusanya Sh11 bilioni.

Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatey Maasay amesema suala la mikataba ya ujenzi wa barabara ya lami kutoka Karatu, Mbulu, Haydom hadi Sibuti, siyo kiini macho kwani utekelezaji wake utafanyika na watengenezaji watarudi.

"Nimeizungumzia mno hii barabara na kupiga sarakasi hadi bungeni na kampuni ya Mwananchi Communications LTD walitoa picha yangu nikifanya hivyo, msijali barabara itajengwa," amesema Maasay.


Mbunge wa Mbulu mjini, Zacharia Paul Isaay amesema maendeleo mengi yamefanyika eneo hilo hata kwenye miradi ambayo haikuandikwa na kuahidiwa kwenye ilani ya uchaguzi.

"Kwa miaka hii minne Serikali ya awamu ya sita imefanya mambo mengi makubwa ambayo hatukutegemea kama yangefanyika tena kwa muda mfupi," amesema Isaay.

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Yustina Rahhi amewasihi wanawake kujitokeza kugombea ubunge wa majimbo na udiwani kwenye kata mbalimbali.

"Wanawake ni jeshi kubwa hivyo mkagombee ubunge wa majimbo na kata, mambo ya viti maalumu waachieni wengine," amesema Rahhi.

Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Mbulu, Marikiadi Nari amempongeza mkuu huyo wa wilaya kwa namna alivyoandaa usomaji wa ilani hiyo kwa kutumia picha jongefu na picha mnato.

"Taarifa hii ikionyeshwa kwa ngazi ya kata na vijiji itasaidia kutoa elimu kwa jamii na kuona maendeleo makubwa kwenye sekta mbalimbali iliyofanywa kupitia serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan," amesema.