Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbinu zitakazosaidia bunifu zinazofanyika nchini kuleta tija kwa jamii

Washindi wa shindano la Wanasayansi Chipukizi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa tuzo zao. Picha: Michael Matemanga.

Muktasari:

  • Ongezeko la rasilimali fedha, uboreshaji wa miundombinu na ujuzi wa teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kwa vijana, pamoja na ushirikiano kati ya Serikali , sekta binafsi na wadau mbalimbali wa maendelea yametajwa kama baadhi ya mambo yatakayosaidia kuendelezwa kwa bunifu zinazofanyika nchini.

Dar es Salaam. Ongezeko la rasilimali fedha, uboreshaji wa miundombinu na ujuzi wa teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kwa vijana, pamoja na ushirikiano kati ya Serikali , sekta binafsi na wadau mbalimbali wa maendelea yametajwa kama baadhi ya mambo yatakayosaidia kuendelezwa kwa bunifu zinazofanyika nchini.

Pia wabunifu, watafiti pamoja na jamii kunufaika na tafiti pamoja na bunifu hizo.

Hayo yamebainishwa Septemba 18, 2025 na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu na teknolojia katika Kongamano la 15 la Shirikisho la Wanasayansi Chipukizi (YST).

Akizungumza katika kongamano hilo, Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Profesa Charles Kihampa amesema vijana katika ngazi mbalimbali za kielimu wamekuwa wakifanya bunifu katika sekta mbalimbali.

Kihampa amesema baadhi ya mawazo ya bunifu hizo ni makubwa na yanaweza kuleta suluhu ya changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii.

Amesema kuwa ili bunifu hizo ziweze kuleta tija kwa jamii zinatakiwa kuendelezwa.

Hivyo ametoa wito kwa sekta binafsi na wadau wengine wa maendeleo kushirikiana kuhakikisha Serikali kuhakikisha bunifu zinazofanyika nchini zinaendelezwa na kusaidia kutatatua changamoto za mbalimbali za kijamii.

“Ili nchi iwe na maendeleo inahitaji kuwa na rasilimaliwatu bora yenye maarifa na ujuzi elimu inayohusha pia maarifa na ujuzi katika sayansi, teknolojia, ubunifu kuchagiza maendeleo endelevu yanayotokana na mtaji wa rasilimaliwatu hiyo”amesema.

Vilevile ametumia fursa hiyo kuhimiza matumizi ya teknolojia katika kurahisisha ufanyaji wa shughuli mbalimbali, kuokoa muda na gharama.

“Kwa mfano nilipotembelea baadhi ya bunifu zilizofanywa na wanafunzi hawa baadhi walikuwa wamebuni mifumo inayosaidia kuchaka na kutafsiri data kwa urahisi ni moja ya faida za teknolojia”anasema.

Kwa upande wake Mwanzilishi mwenza wa shirikisho hilo (YST), Dk Gozibert Kamugisha anamesema kuna wanasayansi chipukizi ambao wamefanya bunifu mbalimbali.

Kamugisha anasema changamoto inayojitokeza ni wapi vijana hao wanaweza kuonyesha bunifu zao ili waweze kusaidiwa kuziendeleza na hata kuja kuleta tija kwa jamii.

“Hapo ndipo tulipoona umuhimu wa kuja na jukwaa ambalo litawasaidia wanasayansi chipukizi kuonyeshwa bunifu zao na kusaidiwa kuziendeleza”anasema.

Amesema tangu walipoanzisha jukwaa hilo sasa ni miaka 15 ambayo imesaidia baadhi ya vijana kuendeleza binifu zao ambazo zimesaidia hata kutengeneza fursa kwa wengine.

Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa wadau kushirikiana na serikali kuhakikisha inawaendeleza vijana wanaofanya bunifu na gunduzi mbalimbali.

Kongamano hilo liliambatana na hafla ya utoaji zawadi kwa wanafunzi wa sekondari waliofanya bunifu zinazoweza kuongeza tija katika sekta mbalimbali ya maendeleo ambapo Shule ya Sekondari ya St Joseph Cathedral iliibuka kidedea.