Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MAWAIDHA: Hatua za ufanyaji wa ibada ya Hijja

Baada ya kufika Makka, hujaji ataelekea moja kwa moja katika Al-Kaaba tukufu kwa ajili ya kufanya tawafu ya Umra au tawafu ya kuwasili.

Akiiona Al-Kaaba, ataleta takbiri na tahlili. Kisha atasimama mbele ya Al-Kaaba, upande wa Hajar Aswad (Jiwe jeusi tayari kwa kuanza tawafu.

Hijja ya Ifraad ni kutia nia ya Hijja pekee bila Umra. Anapoingia Makka, hufanya Tawafu ya Kuwasili mara saba kisha anaswali rakaa mbili nyuma ya Maqam Ibrahim.

Baada ya hapo, yupo huru kuchagua kati ya Kufanya sa’yi baada ya Tawafu ya Kuwasil, au kuichelewesha hadi baada ya Tawafu ya Ifaadha (ya nguzo). Baada ya kukamilisha hayo, anabaki katika hali ya ihramu hadi kuanza kwa ibada za Hijja tarehe nane (siku ya Tarwiya) kwa kuelekea Mina.

Ibada ya Hijja huanza rasmi siku ya Tarwiya, ambayo ni tarehe 8 ya mwezi wa Dhul-Hijja (Mfungo tatu). Katika siku hii, Hujaji anayehiji aina ya Hijja ya Ifraad na Qiraan huenda Mina wakati wa asubuhi.

Hali kadhalika, anayehiji aina ya Tamattui huenda Mina, lakini ni baada ya kutia nia tena ya Hijja. kwa kuwa alikuwa ametoka kwenye Ihram baada ya kumaliza Umra. Inapendekezwa (Sunna) kwa anayekwenda Mina kuoga, kisha avae nguo za Ihram. Ikiwa amenuia aina ya Hijja ya Tamattui, na azidishe kuleta Talibiyya. Huko Mina, ataswali swala ya Aduhuri, Alasiri, Magharibi, Isha, na Al-fajiri. Anaweza kufupisha sala zenye rakaa nne na kuziswali mbili, lakini bila kuzikusanya pamoja.


Siku ya Arafa

Jua linapochomoza katika siku ya tarehe tisa, hujaji ataenda Arafa. Ni muhimu kuhakikisha yuko ndani ya mipaka ya Arafa, kwa kuwa Hijja ni Arafa. Hii ni nguzo kuu ya ibada ya Hijja, na Hijja haiwi sahihi bila kusimama Arafa. Ikiwa mtu hakusimama Arafa, hawezi kulipa ibada hii kwa njia nyingine, wala haitoshelezi kwa kuchinja au kufunga.

Huko Arafa, ataswali Adhuhuri na Alasiri kwa kuzikusanya pamoja kwa (Jam Taqdim) na kwa kuzifupisha. Hujaji atakaa Arafa hadi jua litue, na si lazima kuwa na twahara wakati wa kusimama katika eneo la Arafa.

Baada ya jua kutua, hujaji ataondoka Arafa kuelekea Muzdalifa. Ni Sunna kuswali huko sala ya Magharibi, Isha, na Alfajiri, kisha akae kwa ajili ya kuleta dua na dhikr hadi karibu na kuchomoza kwa jua la siku ya tarehe kumi.

Kwa mujibu wa madhehebu ya Kishafi na Kihanbali, ni wajibu kulala Muzdalifa. Hata hivyo, ni ruhusa kuondoka baada ya katikati ya usiku kwa mahujaji dhaifu wanawake na wagonjwa.

Katika siku ya tarehe kumi siku ya Sikukuu, ndiyo hufanyika ibada nyingi za Hijja, kama vile kurusha mawe Jamara ya Aqaba, kuchinja Hady (mnyama), kunyoa kichwa, na kufanya Twawafu ya Ifadha (tawafu ya Nguzo).

Hujaji anayechinja mnyama wa Hady ni yule aliyetia nia ya aina ya Qarin au Tamattui. Kwa sasa, wengi hulipa gharama ya mnyama wa Hady kupitia taasisi za hisani zinazochinja na kugawa nyama kwa maskini.

Kunyoa nywele hufanyika kwa kutumia wembe, na kupunguza hufanywa kwa mkasi au vinginevyo, mradi tu kinachopunguzwa ni baadhi ya nywele. Kunyoa ni bora zaidi. Mwanamke hukata kiasi cha unywele wake kadiri ya ncha ya kidole. Twawafu ya Ifadha huitwa pia Twawafu ya Ziara au Twawafu ya nguzo.

Inahitaji mtu awe na twahara, kwa kuwa ni kama Sala, isipokuwa inaruhusiwa kuzungumza ndani yake. Twawafu ya nguzo hufanywa kwa kuizunguka Ka‘aba mara saba, kuanzia na kumalizia kwenye Hajar Aswad, huku Ka‘aba ikiwa upande wa kushoto wa mzungukaji.

Kisha Hujaji husali rakaa mbili za Sunna na atafanya Sa‘y (atatembea haraka haraka) baina ya kilima cha Safa na Marwa mara saba, kuanzia kilima cha Safa kumalizia Marwa. Kurusha Mawe Jamara ya Aqaba. Jamara zipo tatu, lakini katika Siku ya kuchinja hurushwa Jamara moja tu, nayo ni ile iliyo karibu zaidi na Makka, iitwayo Jamara ya Aqaba Kubwa.

Hurushwa kwa vijiwe saba mfululizo si kwa pamoja na inapendekezwa kusema “Allahu Akbar” kwa kila kijiwe. Vijiwe hivi huchukuliwa mahali popote.

Matendo matatu haya (kurusha vijiwe Jamara, kunyoa au kupunguza nywele, na Twawafu ya nguzo) yanapofanywa mawili tu kati ya haya (kurusha na kunyoa au kupunguza), basi Hujaji huruhusiwa kufanya baadhi ya mambo yaliyoharamishwa kwake. Hali hii huitwa (tahallul ndogo).

Katika hali hii, huruhusiwa kufanya kila kilichokuwa haramu kwa mwenye kuhiji isipokuwa tendo la ndoa. Akifanya vitendo vyote vitatu (pamoja na tawafu ya nguzo), hutoka kikamilifu (tahallul kubwa) na huruhusiwa kila kitu hadi tendo la ndoa. Baada ya kutekeleza hayo.

Hujaji hupiga kambi Mina na kulala huko siku tatu za Tashriq ambazo ni tarehe 11, 12, kwa mwenye haraka, na 13 kwa asiyeharakisha kuondoka.

Lakini ni bora zaidi kuchelewa kuondoka hadi siku ya 13. Allah Mtukufu anasema “Na mkumbukeni Mwenyezi Mungu katika siku zilizohesabiwa; basi atakayetangulia kuondoka katika siku mbili, si dhambi juu yake, wala atakayekawia, si dhambi juu yake...” (Quran 2: 203).