Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Matumizi bora ya nishati kuondoa upungufu wa umeme

Mwakilishi kampuni ya Sila Afrika akionyesha mifumo ya kudhibiti matumizi ya umeme

Muktasari:

  • Wizara ya Nishati, Umoja wa Ulaya pamoja na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), wameanza majaribio ya mradi wa matumizi bora ya nishati kwa kuzijengea uwezo wa namna ya kufanya tathmini ya matumizi ya nishati na kudhibiti matumizi ya umeme kwa taasisi na viwanda nchini.

Dar es Salaam. Wakati mgao wa umeme ukiendelea kuathiri sekta nyingi nchini, matumizi bora ya nishati iliyopo ni miongoni mwa mipango inayoandaliwa na Serikali kutatua adha ya ukosefu wa umeme.

Matumizi sahihi ya umeme, ni njia inayotajwa kuupunguzia mzigo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuzalisha nishati inayotumika na itakayopotea.

Tayari mradi wa matumizi sahihi ya nishati unatekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa thamani ya Sh 24.18 bilioni (Euro milioni 9)

Kupitia mahojiano na Mwananchi Digital leo 20 Septemba 2023, Mtaalamu Mshauri mradi wa matumizi ya nishati bora kutoka UNDP, Robert Washija amesema moja wapo ya changamoto za mgao wa umeme wamebaini kiasi kinachozalishwa hakitumiki vizuri.

Amesema kutokana na tatizo hilo, mradi wa mataumizi ya nishati bora tayari umeanza kwa majaribio kwenye taasisi mbalimbali na viwanda.

 “Lengo la mradi huu ni kuhakikisha upatikanaji rahisi na endelevu wa nishati ya umeme nchini, tayari tumeshatoa mafunzo kwa taasisi na viwanda vitatu namna ya kufanya tathmini ya matumizi ya nishati, japo mradi huu utakuwa nchi nzima sasa tumeanza kwa majaribio na taasisi za Aga khan, Silaafrica Ltd na PSSSF Complex,” amesema.

Amesema kupitia mradi huo wanakusudia kutengeneza utaratibu wa kitaifa wa matumizi ya nishati katika biashara na majengo makubwa.

Kwa upande wake Mtaalamu wa ukaguzi ufanisi wanishati majengo na mitambo Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) , Agustino Alfred amesema ni muhimu jamii kuwa na matumizi ya nishati  bora ili kutunza mazingira na kupunguza mzigo kwa Tanesco kuzalisha nishati.

 “Nishati tunayozalisha hatuitunzi, kama kiwango cha nishati tunayozalisha upotevu umekuwa mkubwa kunalazimisha Tanesco kuwa na miundombinu ya kuzalisha nishati inayotakiwa kutumika na ile inayopotea,

Kwa hiyo tukitumia nishati vizuri uhitaji wa Tanesco kuzalisha nishati inayopotea inapungua,” amesema.

Takwimu za mwaka 2022 zinaonyesha, Tanesco imepoteza wastani wa Sh 1.2 trilioni sawa na wastani wa Sh300 bilioni kwa mwaka kutokana na upotevu wa umeme ukichangiwa na uchakavu wa miundombinu.