Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mamilioni yatengwa kudhibiti ukatili kwa wafanyakazi wa ndani

Muktasari:

  • Licha ya mchango wao mkubwa kwenye familia, wafanyakazi wa ndani hujikuta wakifanyiwa vitendo vya ukatili na unyanysaji kijinsia kutoka kwa wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki.

Mwanza. Licha ya mchango wao mkubwa kwenye familia, wafanyakazi wa ndani hujikuta wakifanyiwa vitendo vya ukatili na unyanysaji kijinsia kutoka kwa wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki.

Ili kukabiliana na vitendo hivyo, Shirika lisilo la Kiserikali la WoteSawa la jijini Mwanza kwa ufadhili wa Bill & Melinda Gates Foundation linatekeleza mradi wa mwaka mmoja unaogharimu zaidi ya Sh116.4 milioni kuwajengea uwezo wa kujitegemea kiuchumi wafanyakazi wa ndani 150 kutoka Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, Nyamagana na Sengerema mkoani Mwanza.

Ofisa Miradi wa Usawa kwa Wanawake Wafanyakazi wa nyumbani kutoka WoteSawa, Demitila Faustine alisema mradi huo pia utahusu uelewa wa masuala ya uzazi, huduma za afya, uongozi, ushiriki wa wanawake katika maamuzi na usawa wa kijinsia katika masuala ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.

“Kupitia mradi huu, tutawaelimisha na kuwajengea uwezo viongozi wa Serikali za Mitaa, Watendaji wa Kata, Maofisa Ustawi wa Jamii, Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi na makundi mengine ya kijamii kuwawezesha kushiriki vema vita dhidi ya ukatili na unyanyasaji dhidi ya wanawake wafanyakazi wa nyumbani,” alisema Demitila

Alisema mradi huo ulioanza Machi, mwaka huu unatarajiwa kukamilika Machi, mwakani.