Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo manne yanayosumbua watu kisheria

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 20, 2025 jijini Dodoma. Picha na Rachel Chibwete

Muktasari:

  • Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro ametaja mambo manne ambayo yamejitokeza kwa kiasi kikubwa kwenye kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia ambayo ni ukatili wa kijinsia, mirathi, migogoro ya ndoa na migogoro ya ardhi.

Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro ametaja mambo makubwa manne ambayo yamejitokeza kwenye kampeni za msaada wa kisheria wa Mama Samia inayofanywa na wizara hiyo kwenye mikoa mbalimbali nchini ambayo ni vitendo vya ukatili wa kijinsia, migogoro ya ndoa, mirathi na migogoro ya ardhi.

Dk Ndumbaro ameyasema hayo leo Jumatatu Januari 20, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kuhusu kampeni hiyo kuingia kwenye mikoa sita na kufanya mikoa iliyofikiwa kuwa 17 mpaka sasa.

Amesema kwenye maeneo ambayo kampeni hiyo imepita imekutana na malalamiko mengi kuhusu ukatili wa kijinsia na masuala la mirathi, ambapo amewashauri Watanzania kuandika wosia ili kujiepusha na migogoro hiyo.

"Kuhusu watu kuandika wosia wanadhani kuwa wanajitabiria kifo, lakini kuandika wosia kunasaidia kupunguza migogoro ya mirathi kwa sababu nakumbuka miaka 20 nyuma wakati mimi ni mwanasheria niliwahi kumsaidia mzee mmoja kuandika wosia akiwa hoi kitandani lakini mpaka sasa yupo hai na watoto wake wawili wameshafariki, hivyo siyo kweli kuwa kuandika wosia ni kujitabiria kifo," amesema Dk Ndumbaro.

Amesema jambo jingine lililojitokeza ni migogoro ya ndoa, talaka na mgawanyo wa mali ambapo watu wengi wapo kwenye migogoro ya ndoa isiyokwisha huku wengine wakiibuka na migogoro ya ardhi.

Amesema sekta ya ardhi imekuwa na ubabaishaji mkubwa na wakati mwingine imesababisha kuwa na makosa ya jinai na wizara hiyo inajipanga kutatua migogoro ya ardhi, pindi kampeni ya sasa itakapokamilika.

Amesema kuwa wameshawasiliana na Wizara ya Ardhi kuona ni namna gani wataweza kufanya kampeni ya kutatua migogoro ya ardhi tu mpaka imalizike kabisa, kwani inachangia kwa kiasi kikubwa migogoro mingi hapa nchini.

Mbali na hilo amesema mpaka sasa kampeni hiyo imeshafanyika kwenye mikoa 11 na itakapofika Januari 24 mwaka huu wataanza kampeni kwenye mikoa sita mingine ambayo ni Kigoma, Kilimanjaro, Geita, Katavi, Tabora na Mtwara.

Amesema katika kampeni hizo wataalamu wa sheria watakwenda kwenye 10 za kila halmashauri ambapo watahudumia wananchi wenye changamoto za kisheria kwa siku tisa kwenye kila Kata.

Amesema mpaka sasa kampeni hiyo imewahudumia wananchi 775,119 na takribani mashauri 3,162 yametatuliwa.