Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Malecela awataka Wanaccm kuwa wazalendo, kujituma

Muktasari:

  • Makamu mwenyekiti wa zamani wa CCM, John Malecela leo Alhamisi amefanya mazungumzo na katibu mkuu wa chama hicho, Dk Emmanuel Nchimbi na kuwataka wanachama wa chama hicho kuendeleza mshikamano na kuimarisha uongozi wa chama hicho.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu mstaafu, John Malecela amewataka wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kuendelea kuwa na moyo wa kizalendo na kujituma kwa ajili ya maslahi ya Taifa.

Malecela amesema mafanikio ya Serikali katika sekta za maendeleo ya miundombinu, afya, na elimu yanapaswa kuwa chachu ya wanachama wa CCM kuendeleza mshikamano na kuimarisha uongozi wa chama hicho kilichojengwa kwa misingi imara ya kutumikia watu.

Malecela ambaye mbunge wa zamani wa Mtera (Mvumi) mkoani Dodoma ameeleza hayo leo Alhamisi, Desemba 5, 2024 alipotembelewa nyumbani kwake Upanga, jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi.

“Wanachama wa CCM wanapaswa kuwa mfano bora wa uzalendo kwa wengine. Hili ni jukumu letu la kihistoria ambalo tunapaswa kuliheshimu kwa vitendo,” amesema Malecela katika taarifa kwa umma iliyotolewa na CCM.

Pia, mwanasiasa huyo mkongwe aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, amekipongeza chama hicho tawala kwa kuendelea kuonyesha uongozi imara chini ya uenyekiti wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Katika mazungumzo hayo, Malecela ametoa wito kwa wanachama wa CCM kuendeleza mshikamano na maadili ya chama, akisisitiza kuwa ni mojawapo ya misingi ya mafanikio ya CCM kwa zaidi ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwake.

Amewaasa viongozi wa sasa wa CCM kuendeleza kazi nzuri wanayoifanya, huku wakizingatia misingi ya haki, uwazi, na uwajibikaji. Amesema maadili ya uongozi bora yamekuwa kichocheo kikubwa cha imani ya wananchi kwa CCM.

“Huu ni wakati wa kuchapa kazi zaidi, kuhakikisha tunazidi kuimarisha maendeleo ya nchi yetu, huku tukiheshimu dhamira kuu ya chama ya kuwatumikia wananchi,” amesema Malecela.

Kwa upande wake, Dk Nchimbi amemshukuru Malecela kwa mchango wake wa mawazo na uzoefu unaoendelea kuwa hazina kubwa kwa CCM na Serikali.

Amesema viongozi wastaafu kama Malecela wamekuwa mstari wa mbele kutoa ushauri unaosaidia kuimarisha utendaji wa chama hicho katika nyanja mbalimbali.

“Uzoefu wenu ni mwanga kwetu. Tunaendelea kuthamini mawazo yenu ambayo yamekuwa nguzo muhimu kwa chama na Taifa kwa ujumla,” amesema Dk Nchimbi.