Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makonda amchangia Profesa Jay Sh20 milioni

Muktasari:

  • Makonda na ndugu zake wametimiza ahadi ya kumchangia Sh20 mwanamuziki mkongwe wa kizazi kipya, Profesa Jay kwa ajili ya kutunisha mfuko wa taasisi ya kusaidia wagonjwa wenye matatizo ya figo nchini

Dar es Salaam. Katibu wa Halmshauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda amemchangia Sh10 milioni mwanamuziki Joseph Haule maarufu ‘Profesa Jay’.

Pia, Makonda amemkabidihi Profesa Jay Sh10 milioni nyingine ikiwa ni mchango kutoka kwa ndugu zake (Makonda) na kufikia jumla ya Sh20 milioni.

Makonda ametoa kiasi hicho leo, Desemba 22, 2023 alipokwenda nyumbani kwa msanii huyo Mbezi, Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni kutekeleza ahadi yake binafsi  aliyoitoa siku uzinduzi wa taasisi ya  mwanamuziki huyo ya kusaidia wagonjwa wa figo.


Akizungumza baada ya kukabidhi fedha hizo, Makonda ameeleza changamoto anayopata Profesa Jay kwenda na kurudi kutoka Mbezi hadi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuahidi kumtafutia nyumba na kumlipia eneo la Upanga, ili kuepukana na changamoto hiyo.

Makonda pia amemuahidi msanii huyo kumsaidia kuwakumbushia wale wote walioahidi kumchangia kukamilisha ahadi zao.

Profesa Jay ameanzisha taasisi hiyo kwa lengo la kuwasaidia wengine baada ya kusumbuliwa na tatizo la figo kwa miaka miwili na amekuwa akitumia gharama kubwa kupata matibabu.

Siku ya uzinduzi wa taasisi hiyo, Rais Samia Suluhu Hassan alimuunga mkono kwa kumuahidi kuchangia kwenye mfuko huo Sh97 milioni.