Majina 19 ya waliopoteza maisha ajali ya ndege haya hapa

Muktasari:
Kesho Jumatatu, Novemba 7, 2022, miili ya watu 19 waliopoteza maisha katika ajali ya ndege ya Shirika la Precision Air, baada ya kuanguka Ziwa Victroria, Bukoba mkoani Kagera, itaagwa katika Uwanja wa Kaitaba na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ataongoza shughuli hiyo.
Dar/Bukoba. Mkuu wa Mkoa wa Kagera (RC), Albert Chalamila ametaja majina 19 ya watu waliopoteza maisha kufuatia ajali ya ndege ya Shirika la Precision Air iliyoangukia Ziwa Victoria mkoani humo asubuhi ya leo Jumapili, Novemba 6, 2022.
Chalamila ametaja majina hayo mbele ya waandishi wa habari ambao ni;
1 Atulinde Biteya
2. Aneth Biteya
3. Neema Faraja
4. Hanifa Hamza
5. Aneth Kaaya
6. Victor Laurean
7. Said Malat Lyangana
8. Iman Paul
9. Faraji Yusuph
10. Dk Boniface Jullu
11. Sauli Epimark
12. Zacharia Mlacha
13. Eunice Ndirangu
14. Mtani Njegere
15. Zaituni Shillah
16. Dr. Alice Simwinga
17. Buruani Bubaga – Rubani
18. Peter Odhiambo - first officer.
19. Mmoja ni sista hajatambulika jina lake
Ndege hiyo aina ya Air ATR 42 mali ya Precission Air ilikuwa ikitokea jijini Dar es Salaam kwenda Bukoba.
Mkuu huyo wa mkoa amesema tayari Waziri Mkuu Kassim Majaliwa yupo mkoani Kagera kuungana na wananchi wa mkoa kuaga miili ya watu waliopoteza maisha kufuati ajali hiyo akimwakilisha pia Rais Samia Suluhu Hassn.
Amesema ratiba ya misa ya kuaga miili ya wote waliopoteza maisha itaanza saa nne asubuhi katika Uwanja wa Kaitaba ambapo dua na sala zitaendeshwa na viongozi wa dini ya Kiislamu na Kikristo.
Mara baada ya kuwasili mkoani humo, Majaliwa amesema,”Rais Samia ameniagiza kuja kufuatilia zoezi hili na kuhakikisha linakwenda salama, pia ameguswa sana na tukio hili, na amekuwa akifuatilia kwa karibu ili kuhakikisha zoezi la uokoaji linafanyika kwa mafanikio.”
Majaliwa amesema abiria 26 wameokolewa na kukiwa na miili 19 ambayo imetolewa katika eneo la ajali.