Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mahawanga ahoji elimu ya mlipakodi kwa wanawake

Naibu waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande akijibu maswali ya wabunge leo Aprili 11,2025 bungeni Jijini Dodoma. Picha na Hamis Mniha

Muktasari:

  • Mbunge ataka wanawake wapewe elimu ya mlipa kodi ili watambue wajibu wao kwenye eneo la kodi.

Dodoma. Mbunge wa Viti Maalumu, Janeth Mahawanga ameihoji Serikali ina mpango gani wa kuanzisha madarasa ya Elimu kwa Mlipa Kodi kupitia vikundi vya wanawake wajasiriamali.
Mbunge huyo amesema kutoa elimu kupitia makundi ya wanawake itasaidia elimu ya mlipakodi kuwafikia wahusika moja kwa moja na kutasaidia walipa kodi kutambua wajibu wao.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande amesema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekuwa ikitoa elimu ya kodi kwa njia mbalimbali kwa makundi yote ya walipakodi na vikundi vya wanawake wajasiriamali.

Naibu Waziri amesema, TRA imekuwa ikielimisha wanawake wajasiriamali kupitia vikundi vyao ikiwemo chemba ya wafanyabiashara wanawake “Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC)” na makundi mengine ya wajasiriamali wanawake.

Amesema katika kuhakikisha uendelevu katika kuwafikia wajasiriamali wanawake, TRA itaendelea kushirikiana kikamilifu na wizara husika kuimarisha mawasiliano na mtandao wa wanawake wajasiriamali ili kupitia taasisi au jumuiya zao tuweze kukidhi mahitaji ya elimu ya kodi na shughuli zao za kiuchumi.